Unakumbuka kuna muda google walikuja na akili bandia inayoitwa Bard? Kwa sasa wamekuja na akili bandia ambayo ni kubwa kuliko ya mwanzo ambayo inakwenda kwa jina la Gemini.
Bard ilikuja na kupata sifa kadha wa kaza maana ilikua ni chatbot tuu ambayo inatumia akili bandia lakini kwa sasa google wameongeza uwezo huo kupitia Gemini.
Kuongeza huku kumefanyika kwa kuongezea ili uwezo kuwa mkubwa zaidi na hii ni kwa kupitia Gemini.
Ni wazi kwamba katika upande wa teknolojia Google ni moja kati ya makampuni ambayo yana uwezo mkubwa na wana ubunifu mbalimbali wa kiteknolojia.
Akili Bandi hii itakua na uwezo wa kufanya haya na zaidi
Kutambua picha, maneno, kusoma vitabu, kujibu maswali yanayotumia akili sana, inafanya mahesabu, kutengeneza codes, kuchora, kutengeneza picha, video na sauti n.k
Moja kwa moja akili bandia hii itakua ndani ya simu za Android na itaanza katika Google Pixel 8 Pro. Kwa sasa ni wazi akili bandia zipo za aina nyingi na hii ni baada ya ChatGPT ilipojipatia umaarufu mkubwa.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika sehemu ya comment je unahisi akili bandia hii itakua ni mshindani mkubwa sana kwa akili bandia zingine ambazo zinafahamika
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.