fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Android Intaneti IPhone meseji simu Smartphones Teknolojia

Kuwa Tayari Kwa Emoji Mpya Na Nzuri Zaidi!

Kuwa Tayari Kwa Emoji Mpya Na Nzuri Zaidi!

Spread the love

mobile emojis

Tunaweza tafuta njia mbadala ya kuonyesha Msisimko wetu wakati wa kutuma meseji na kuchati katika vifaa vyetu vya elektroniki. Kutuma meseji kwa kutumia Emoji (Zile alama za rangirangi kama sura ya furaha, ukauzu, kununa, dole gumba n.k) inaweza fanya meseji ikaonekana nzuri zaidi. Mfano ukituma meseji ya kuchekesha alafu mtu akakujibu ujumbe akaweka na zile emoji za sura ya kucheka  ukiachana na ‘hahahahahaha’ inakua inavutia zaidi.

“Watu wote duniani wanahitaji Emoji ambazo zinafanaa zaidi na watu hasa hasa katika swala la rangi za ngozi” Unicode waliandika katika ripoti yao

Ripoti hiyo ni rasimu ya baadae kuhusina na mipango ya kundi hilo kuhusina na Emoji, kwa hiyo inaweza ikabadilika kabla ya mwezi julai mwaka ujao. Unicode imekua ikipoke shinikizo kwa watu mbali mbali na hata kampuni ya Apple kwamba inabidi itengeneze Emoji ambazo kidogo zinafanana na watu wanaozitumia.

SOMA PIA  Tecno Camon 16s ipo Njiani Kuingia Sokoni Hivi Karibuni

Emoji zenye sura mbali mbali zinakuja kabla ya mwezi julai 2015 na hii habari ni kutoka kwa Unicode (kundi la watu wanaosimamia Emoji). Aina 5 tofauti za ngozi zimepangwa kuwepo katika ‘Update’ ya software ya  Unicode katika  Emoji zinayokuja.

Emoji Za 2015 Zinategemewa Kuwa Katika Mfumo Huu

Emoji Za 2015 Zinatarajiwa Kuwa Katika Mfumo Huu

Emoji ambazo zimezoeleka sasa ni zile za watu wenye ngozi nyeupe. vipi kuhusu ngozi nyeusi na zingine?  Emoji mpya zitakua na mabadiliko hata kwa rangi za nywele na hii inavutia zaidi!.

SOMA PIA  Apple yaanzisha programu ya kurekebisha iPhone 12 na 12 Pro bure

Hii ni taarifa nzuri kwa wale wanao lalamika kuhusiana na Emoji kukosa rangi za ngozi mbali mbali. Ukiangali Emoji ni njia mpya ya siku hizi ya watu kuwasiliana, badala ya kuandika maneno unaweza tuma emoji. Wewe umeipokea vipi taarifa hii?? Tuammbie katika Facebook Page Yetu na pia tembelea Instagram Page yetu

SOMA PIA  Huduma za Vodacom Business kwa Biashara Ndogondogo

Siku Njema!!!

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania