fbpx

Unajua undani wa Honor V20?

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Honor ni bidhaa ambazo zipo chini ya Huawei Technologies na ni moja ya simu ambazo zinaiweka kampuni husika kwenye ushindani mzuri kila mara takwimu zinapotolewa.

Huawei wameamua kuanza mwaka 2019 kwa kutoa Honor View 20 (V20) ambayo inatazamiwa kupendwa na wengi kutokana na sifa zake lakini hata bei yake inastahimilika. Sifa za simu yenyewe ni kama ifuatavyo:-

Kipuri mama/Ukubwa wa kioo.

Simu hiyo imewekwakiungo kikuu kabisa kinachofahamika kama Kirin 980; kama moja ya vipuri vya kisasa ambavyo Huawei/Honor wamekuwa wakitumia kwenye runnunu. Upande wa kioo kina urefu wa inchi 6.4 aina ya LCD ubora wa 1080p.

Kamera.

Nguvu nyingi zimewekwa kwenye kamera kama ilivyo kawaida ya simu nyingi za karibuni; Honor V20 ina 25MP kwenye kamera ya mbele ambayo imewekwa upande wa kushoto katika muundo wa tundu dogo ambalo huwezi kulihisi unapogusa kamera husika.

INAYOHUSIANA  Ushirikiano kati ya HaloPesa na VISA wazinduliwa

Kwa nyuma kamera kuu ina 48MP Sony IMX586 ikiwa pamoja na kamera nyungine ndogo ya 3D ToF kwa ajili ya kusaidia kupata picha nzuri nyakti za usiku; 3D ToF inaelezwa kuwa na 12MP.

Honor V20

Kamera za kwenye Honor View 20.

Memori ya ndani/RAM.

Hapo wameamua kuwa na aina mbili tofauti GB 6 au GB 8 upande wa RAM huku diski uhifadhi ni GB 128/256GB.

Betri/Uwezo wa kimemeshi.

Betri ya kwenye Honor V20 ina 4000mAh lakini pia una teknolojia ya kuchaji haraka inayopitisha 4.5V/5A kwa maana ya kwamba inachukua takribani dakika 30 kuchaji kutoka asilimia 0-55.

Bei, Rangi na Mengineyo.

Ipo katika rangi tatu; Nyekundu, Nyeusi na Bluu. Bei inatofautiana kulingana na kubwa wa RAM/diski uhifadhi mathalani 6/128GB inagharimu $435|Tsh. 1,000,500, 8/128GB ni $510|Tsh. 1,173,000 na 8/256 ikiuzwa $580|Tsh. 1,334,000. Ina uwezo wa kuwa kompyuta kamili ukiunganisha pamoja na kicharazio, ‘Kipanya’ lakini pia runinga kwa ajili ya kuonyesha vitu vinavyofanyika. Pia, ina antena 3 za Wi-Fi, ina teknolojia ya kuruhusu GPS mbili.

INAYOHUSIANA  Mambo ya kuzingatia katika kuchaji simu na kufanya betri zidumu

Ukiizungushazungusha kwa nyuma utaona mistari fulani fulani ya 3D (tazama picha mnato hapo chini) kitu ambacho kinaifanya kuvutia. Kuzinduliwa kwake kwa duniani kote ni mpaka Januari 22.

Vyanzo: GSMArena, Gizmo China

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.