Aseeeeh!, WhatsApp wanatoa maboresho mengi katika mtandao wao kijamii na ukifuatilia ndani ya kipindi cha miezi miwili tuu nimeandika maboresho na vipengele vipya vingi kutoka kwa mtandao huu.
Mtandao wa WhatsApp ni moja kati ya mitandao maarufu sana ambayo inajihusisha na meseji za papo kwa papo na sasa hivi inakuja na kipengele kipya.
Fikiria ukiwa unaongea na simu katika mtandao huo alafu ukawa na uwezo wa kufanya vitu vingine na yule unaongea nae ukiachana na kuongea tuu.
Katika kipengele hiki kitu ambacho kitafanyika ni uwezo wa kuweza ku’share muziki kwa kuusikiliza wote —- yaani mmoja anaweza akacheza muziki na pande zote mbili zikawa zinasikiliza muziki huo.
Kingine ni kwamba kipengele hiki kitakua kinakubali katika simu za video tuu na sio simu za sauti (voice calls) kutoka katika mtandao huo.
Kipengele hiki kwa sasa kipo katika hatua za mwanzo mwanzo na kinategemewa kuwa rasmi katika matoleo yajayo ya WhatsApp.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment je umeipokeaje taarifa hii kutoka katika mtandao wa WhatsApp?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.