fbpx
apps, Intaneti, Mtandao wa Kijamii, simu, Teknolojia

Misri: Sheria kali ya udhibiti mitandao ya kijamii

misri-sheria-kali-ya-udhibiti-mitandao-ya-kijamii
Sambaza

Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi, Agosti 18 amesaini sheria mpya ambayo inawabana watu kutumia mtandao ya kijamii kwa kiwango kikubwa.


Lengo la kupitisha sheria hiyo serikali imesema kwamba hatua hiyo mpya ni katika jitihada za kukabiliana na ugaidi na vurugu za aina yoyote ambazo zimekuwa zikisababishwa na uchochezi kupitia mitandao.

Sheria hiyo ya mtandao ina nguvu ya kuzuia tovuti nchini humo ikiwa zinaonekana kuwa tishio kwa usalama wa taifa hilo au uchumi wake.

Mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kuendesha, au kutembelea, tovuti za aina hiyo anaweza kufungwa au kulipishwa faini na kwa mujibu wa gazeti la Al haram limesema faini ya kosa hilo $10,000 au kifungo cha miaka miwili jela.

Taasisi iliyopo Cairo inayoangazia uhuru wa kufikiri na kujieleza imesema zaidi ya tovuti 500 zimeshafungwa hadi sasa nchini Misri tangu mwaka 2017 hata kabla ya sheria hiyo mpya kuanza kutumika.

sheria
Nchini Misri baada ya kufungia maandamano, mitandao ya kijamii ilikuwa ni sehemu pekee ambayo Wamisri walikuwa wanaweza kuikosoa serikali.

Mwezi uliopita mswada mwingine ulipitishwa na bunge la Misri kwamba mtu yeyote ambaye ana marafiki zaidi ya 5,000 kwenye mtandao wa kijamii inabidi awe kwenye uangalizi maalum lakini mswada huo bado haujasainiwa na rais wa nchi hiyo ili kuwa sheria.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Jinsi Ya Ku'Post Picha/Video Ktk Instagram Kwa Kutumia Kompyuta!
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.