fbpx
Facebook, Teknolojia

Facebook Yahifadhi Password za Watumiaji Wake kwa njia isiyo salama

facebook-yahifadhi-password-za-watumiaji-wake
Sambaza

Leo tarehe March 21, 2019 katika tovuti yao ya habari ya Facebook iliyoandikwa na  injinia wa usalama wa mtandao huo wa kijamii  inasema kuwa wamegundua kuwa passwords (Nywila) za watumiaji wa facebook takribani milioni 600 zilihifadhiwa kwa njia ambayo inayosomeka kawaida yani kitaalamu wanaita Plaintext.

Facebook Yahifadhi Password
Facebook

Suala ambalo lilifanyika kimakosa na wafanyakazi zaidi ya 20,000 wa Facebook lilihusisha wafanyakazi hao kutumia programu flani kwenye kompyuta zao za kazini ambayo kimakosa iliweka data za nywila/passwords za watu wanaofungua akaunti katika mtandao huo wa kijamii bila ya kuzilinda. Yaani ilihifadhi nywila kwa mfumo wa document za kawaida za kimaandishi (plain text).

Nywila hizo zimehifadhiwa kwa namna ambayo injia wote wa facebook wenye ruhusa maalumu wanaweza kuona password ambazo watumiaji wanatumia kwa ajili ya kuingia ndani ya akaunti zao. Hii ni jambo lengine baya linalotokea ndani ya Facebook ingawa mpaka sasa mkuu wa usalama wa program hiyo amedai hakuna habari zozote mbaya za matumizi ya Nywila hizo nje ya Facebook.

Injinia wa Facebook amedai data za kiusalama walizonazo zinaonesha hakuna ata mfanyakazi mmoja wa kampuni hiyo alitumia vibaya data hizo za watumiaji.

INAYOHUSIANA  Uchina: Waja na mfumo wa utambuzi wa watu kwa kutambua jinsi wanavyotembea (Surveillance)

Fahamu njia ya kuhakikisha akaunti ya Facebook ni salama zaidi.

TUMIA NJIA HIZI KUIMARISHA ULINZI WA AKAUNTI YAKO

Kwa kufanya hivo sasa unaweza kuondoa mashaka juu ya akaunti yako.

Una mtazamo gani na uzembe huu uliofanywa na Facebook?

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Lymo

A Cyber Security Guy | A student | I Know A lot