EyeQue Check: Kifaa cha kupima macho nyumbani

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

EyeQue ambayo ni kampuni iliyoko Newark, California nchini Marekani imetoa kifaa maalumu kinachoweza kutumika nyumbani kwa ajili ya upimaji wa macho kinachokwenda kwa jina la EyeQue Check.

Kifaa hicho kinachofahamika kama EyeQueCheck ili kiweze kufanya kazi hiyo ya upimaji wa macho inabidi kiunganishwe na skrini ya simu Janja na kisha kuweka jicho lako kwa ajili ya upimaji huo.

  • Simu Janja ndiyo itakayohitajika kwa kuanzia na mfumo wa Android toleo la 4 au iOS 9.3 na kuendelea matoleo ya juu.
  • Itambidi mwenye kifaa hicho kupakua App maalumu ya upimaji kwa kuingia App Store au Google Play Store.
INAYOHUSIANA  Apple wataka simu zao ziwe na uwezo wa kuwa laptop kamili! #Teknolojia

Sambamba na hilo kunakuwa na Programu maalum itakayokuwa inaonesha herufi na picha mbalimbali ili kuweza kubaini tatizo la jicho na kushauri Lens gani inamfaa mpimaji kwa ajili ya miwani.

EyeQue Check

EyeQue Check

Kupitia matokeo ya upimaji huo mgonjwa atapata majibu yake ambayo yatamuwezesha kwenda kwenye Kliniki za utengenezaji vioo maalumu vya macho kwa uvaaji wa Miwani.

Kifaa hicho pia kinawezesha daktari wa macho kupima mgonjwa bila kuwa karibu naye.

INAYOHUSIANA  Ehang 184; Drone yenye Uwezo wa kubeba Abiria

Kadhalika, kinakushauri kuhusu aina ya miwani itakayofaa kuvalia unapokuwa na matatizo ya macho bila ushauri wa daktari. Kinatumia programu (app) kukutumia matokeo katika simu kwa njia ya Intaneti.

Kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani (WHO) linakadiria kuwa zaidi ya watu 1.3 bilioni wana shida ya macho duniani.

Watu milioni 89 wana matatizo madogo madogo ya macho. Watu milioni 217 wana matatizo makubwa na watu milioni 36 ni vipofu.

INAYOHUSIANA  Jinsi Ya Kufufua Mafaili Yaliyofutwa Katika Simu/Kompyuta!

Soma makala mbalimbali za teknolojia katika sekta ya afya – Teknokona/Afya

Shirika hilo linasema kuwa asilimia 80 ya matatizo ya macho yanaweza kuepukika. Inapendekeza watu wapimwe macho kila baada miezi sita au mwaka mmoja ili kuepuka upofu unaoweza kuepukika.

Kwa mwenye kupenda kuwa na EyeQueCheck anaweza kununua kwenye mtandao wa Amazon kwa kiasi cha Dola 70 takribani sawa na Tshs 160,000/-

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.