Katika mtandao vile vile faragha (Privacy) ni kitu muhimu sana kukitilia maanani na hiki ni moja kati ya vipengele ambacho kinayapa sifa kubwa makampuni, sasa hivi Gmail wamegoma kusalia nyuma.
Google inakuaja na teknolojia hii katika huduma yake barua pepe (email) yaani Gmail, ni wazi kuwa kampuni imekua ikiandaa kuwezesha kipengele cha ‘End-To-End Encryption’ katika mtandao wake kwa muda sasa.
Ndani ya Gmail ukiachana na mtumaji na mpokeaji wa barua pepe hiyo basi hakuna mtu mwingine yeyote ambae ataweza kuona kilichotumwa.
Yaani kuanzia eneo la subject mpaka kilichopo ndani hakitaonekana hata kwa timu nzima ya Gmail, ukiachana na hayo hata viambata (attachment) havitaonekana.
Ubaya wake ni kwamba kwa sasa huduma hii inapatikana katika Gmail ya kwenye mtandao tuu (kompyuta) na kwa sasa iko katika hatua ya majaribio?
Teknolojia hii inalinda kwa kiasi kikubwa faragha ya kile kilichotumwa tena ni nzuri zaidi kwa wale ambao wanafanya biashara kama makampuni n.k.
Kwa sasa ni wateja wa huduma ya Google kutoka Google Workspace Enterprise Plus, Education Plus na Education Standard ndio wanaweza kupata toleo la majaribio tena ni kwa kuomba kujaribu toleo hilo mpaka kufikia januari 20.
Pia wateja wa kawaida (gmail ya kawaida) hawajasahaulika na huduma hii itakua ikifanya kazi mpaka katika Google Drive, Google Docs, Sheets, Slides, Google Meet, na Google Calendar (toleo la beta) kwa maana huduma hizi zinaingiliana moja kwa moja na Gmail.
Soma kila kitu kuhusiana na Gmail >>HAPA<<
Ni wazi kwamba Google huwa inatumia muda mwingi sana katika kuhakikisha kuwa wateja wake wanapata kile kilicho bora zaidi na hili wanalifanya kwa njia nyingi ikiwemo na kuhakikisha kuwa wanawaletea matoleo mapya (masasisho) na kuboresha huduma.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je hii umeipokeaje unadhani kulikua na umuhimu wa kuleta kipengele hiki katika huduma hiyo?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.