Ni kitu ambacho labda tunakiona kila siku, je maana yake dhahiri tunaifahamu? Wengi ‘End-to-end Encryption’ kwa kiasi kikubwa ipo katika mitandao mingi ya kijamii ambayo inajikita katika kutuma na kupokea jumbe za mawasiliano.
Kwa mfano katika mtandao wa WhatsApp natumai wengi mnaona teknolojia hii ikiwepo kwa kiasi kikubwa. Hii maana yake ni nini sasa? leo TeknoKona inakujulisha zaidi juu ya teknolojia hii.
Maana halisi ya teknolojia ya ‘End-to-end Encryption’ ni kwamba hii inamuhakikishia mtumaji wa taarifa (ujumbe) kuwa taarifa hiyo itaenda moja kwa moja kwa muhusika bila ya mtu yeyote wa katika kuisoma taarifa hiyo.
Kwa lugha ya kawaida kabisa ni kwamba teknolojia hii inalinda taarifa unazotuma zisiweze somwa na mtu mwingine yeyote usipokuwa yule ambae amekusidiwa. Hii inamaana kuwa hata wale ambao wanamiliki mtandao husika (mfano WhatsApp) hawataweza soma taarifa hiyo.
TUINGIE NDANI KIDOGO: Encryption Ni Nini?
Ujumbe ukiwa ‘Encrypted’ inamaanisha umefungwa katika hali ya kwamba mpaka mtu awe na ufunguo (Decrepted) ndio anaweza kufungua na kusoma ujumbe huo.. fikiria kama kuloki mlango na funguo ni lazima mtu awe na funguo ndio aweze kuingia ndani.
Kwa haraka haraka hivi ndio inavyobidi teknolojia ya ‘Encryption’ inavyofaya kazi. Hii pia ina maana kuwa kuna zingine zinakuwa na ubora kuliko zingine.. inategemeana na jinsi tuu teknolojia hizo zinavyotelewa na kampuni husika
Teknolojia hii ya uficho vifaa vyetu vinaitumia kila siku ila ni ngumu kujua kwa haraka haraka kwa mfano tovuti nyingi zinazotumia mfumo wa HTTPS, kama vile zile za mabenki ni kwamba kunakuwa na uficho wa taarifa kati yako wewe na benki husika ila kumfanya mtoaji wa huduma ya intaneti (mfano Tigo, Vodacom, TCCL n.k) asiweze soma taarifa hizo mfano neno siri na taarifa za fedha.
Kumbuka kwa hapo tulikua hatuongelei ‘End-to-end encryption’ bali namna ya ‘encryption’ inavyofanya kazi.
KWANINI End-to-end encryption ?
Ni wazi kuwa teknolojia hii inasaidia sana katika swala zima la usiri. Vtu vyote ambavyo ni vya siri unaweza wasilisha kwa mtu kwa kutumia njia au teknolojia hii huku ukiwa unajiamini kuwa katikati za zoezi hilo haviwezi kudukuliwa.
Ukiwa unatuma ujumbe kwa mfano katika mtandao na ujumbe huo hauko katika mfumo wa ‘End-to-end encryption’ hapo ni wazi kuwa ujumbe huo unaweza somwa na mtandao husika. Kwa mfano kama kwenye mtandao wa WhatsApp teknolojia hii haujaiwasha wewe na yule unaemtumia ujumbe ni wazi kwamba WhatsApp waanaweza soma taarifa mnazotumiana
‘End-to-end encryption’ vile vile inasaidia sana katika swala la kujiamini katika mitandao kumbuka taarifa kama zile za hospitali, benki n.k zinaweza zikawa zinatumwa na kupokelewa kwa urahisi na usalama zaidi.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika sanduku la maoni.. wewe hii umeipokeaje? na je teknolojia hii umekuwa ukiitumia mara kwa mara au bado? karibu!
Soma makala zingine za ujanja ujanja -> Teknokona/Maujanja
No Comment! Be the first one.