Vifaa vya Playstation vimefanya sana vizuri katika soko na bado vinaendelea kufanya hivyo. Playstation 5 nayo imefanya vizuri sana katika upande wa mauzo na kila kitu.
Kwa sasa fununu ni nyingi kwamba kampuni hiyo inayomilikiwa na Sony ina mpango wa kuachia vifaa vingine ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa PS 5.
Kingine kinachosemekana ni kwamba vifaa hivyo vipya havitakua na tofauti kubwa ya kimuonekano na PS 5 ya sasa.
PlayStation Hardware Roadmap:
-PlayStation VR 2: March 2023
-PlayStation 5 Slim 5nm: September 2023
-PlayStation 5 Pro 5nm/4nm: November 2024#PS5 #PlayStation5 #PlayStation #PlayHasNoLimits #DualSense #PlayStationVR2 #PSVR2 #PlayStation5Slim #PS5Slim #PlayStation5Pro #PS5Pro pic.twitter.com/oSWvMdykbo— @Zuby_Tech (@Zuby_Tech) May 25, 2022
kuna chanzo ambacho chenyewe kimesema kuwa kifaa cha PS 5 Pro kitatoka mwaka 2024 huku kifaa cha PS 5 Slim itatoka mwaka 2023 na matoleo haya yote yatakua hayana tofauti kubwa ya kimuonekano na toleo la sasa.
Kumbuka matoleo hayo mawili vile vile yanategemewa kuwa na umbo dogo ukilinganisha na toleo la sasa maana kampuni imejikita huko kwa sasa.
Kwa sasa haya yote yapo kama fununu maana kampuni ya Sony haijaweka wazi, na ukiachana na hili la kuweka wazi ni kwamba fununu hizi zimekua zikisambaa kwa muda mrefu.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je ushawahi kutumia au unatumia PS 5? Niambie uzoefu wako na kifaa hicho.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.