Je ChatGPT ni nini? Kama bado haujasikia basi fahamu ni moja ya kitu kipya kilichopata umaarufu sana hivi karibuni katika ulimwengu wa teknolojia. Ni zao la teknolojia ya akili bandia ‘AI’ na tayari inazungumziwa kwa upana kwa mitandao ya kijamii na kwenye vyombo vya habari.
ChatGPT ni kitu gani?
Hii ni teknolojia ambayo yenyewe inaweza kusoma, kuelewa na kufanya kazi kama binadamu kwa jina jingine tunaita akili bandia yaani (Artificial intelligence/AI) yaani hii ChatGPT inauwezo wakufanya vitu au mambo ambayo yanahitaji ufahamu wa mwanadamu kama vile kufanya maamuzi, kutatua tatizo, kusoma, nk.
ChatGPT ni akili bandia/AI ambayo imejifunza mifano mingi ya taarifa/data ya maneno, hii imeifanya iweze kuelewa swali na kutoa majibu yenye asili kama ya binadamu.
Uzuri wa hii akili bandia/AI inaelewa lugha nyingi sana pindi utakapoiuliza, yani ukiuliza kiswahili utajibiwa kiswahili na ukiuliza kwa lugha tafauti itakujibu kwa lugha usika.
ChatGPT sio Google kwa sababu;
ChatGPT yenyewe inajibu swali ambalo mtumiaji ameuliza wakati Google yenyewe ni kivinjari/search engine yaani inatafuta/search na inavuta taarifa/data mbalimbali mtandaoni ambazo zinaendana na swali ambalo mtumiaji ameuliza. ChatGPT imetumia na inajiendesha kwenye mfumo wa teknolojia ya AI katika kujifunza mambo na kuweza kujielezea kama vile binadamu (kwa sasa kwa maneno), wakati Google inatumia mfumo wa AI katika utafutaji wa majibu na anuani sahihi za ile kile kitu unataka kufahamu.
Kimsingi ni kama zinataka kufanana ila HAPANA ni vitu viwili tofauti.
Google walipoulizwa kama wanaona ChatGPT itatishia uwepo wao walisema ‘hapana’, ata wao kupitia mradi wao wa LaMDA ambao hivi karibuni ili’trend’ wanasema tayari wana kitu chenye uwezo kama huo au ata zaidi [Soma habari ya teknolojia ya Google hapa -> Injinia wa Google adai Mfumo wa Roboti umepata Hisia, Unajitambua. Google wamsimamisha kazi. Wanaamini pia matumizi ya Google yataendelea kuwa tofauti na vile mtu atatumia teknolojia za AI kama vile ChatGPT au LaMDA.
Unaweza kujiandikisha na kuijaribu kupitia tovuti ya https://openai.com/
Kila siku teknolojia zinavumbuliwa ili kutusaidia na kuturahisishia kazi kwa namna moja au nyingine ili kuendana na ukuaji wa teknolojia husika, ni vyema kuelewa hata kwa uchache haya mabadiliko ya teknolojia ili kujiweka sehemu nzuri zaidi.
Vyanzo: OpenAI, 9to5Google
No Comment! Be the first one.