Injinia adai mfumo wa roboti umepata hisia na kuweza kujitambua na kujipa sifa ya kuwa sawa na mwanadamu. Roboti huyo anayetengenezwa na Google kupitia teknolojia za AI (Akili bandia – artificial intelligence) ni roboti spesheli kwa ajili ya mazungumzo. Madai hayo yameleta mtafaruki kwa wadau wa masuala ya usalama wa kiroboti.

Katika kitu ambacho kinawagawa wanasayansi na wanaharakati wa masuala ya usalama wa kiteknolojia ni hofu ya kwamba kuna hatua itafikiwa ambapo roboti wataweza kuwa na akili ya kujitambua, kujenga mahusiano na kuchukua hatua mbaya dhidi ya utawala wa binadamu. Hivyo madai ya Injinia Blake Lemoine yameleta hofu kama tayari jambo hili limefikiwa kupitia kompyuta roboti anayetengenezwa na kitengo cha Google kinachotambulika kwa jina la Responsible AI.
Kompyuta roboti wa kitengo hicho anayefahamika kupitia jina la mradi – LaMDA, alikuwa anafanyiwa majaribio ya mazungumzo na Injinia Blake. Katika majaribio hayo ndipo kutokana na maswali na majibu aliyopatiwa na roboti huyo yamemfanya Injinia aamini nje ya utaratibu na sheria za kiteknolojia za sasa, inawezekana roboti huyu amefikia hatua ya kujielewa na kuwa na hisia.
LaMDA ni nini?

‘Language Model for Dialogue Applications (Lamda)’ ni teknolojia ya mazungumzo ya uandishi (chatbot) inayohusisha utumiaji wa teknolojia za kisasa zaidi inayoendeshwa kupitia kitengo cha tafiti cha Google. LaMDA imefikia sifa ya kuitwa kitu chenye akili zaidi kuwahi kutengenezwa na mwanadamu.
Wakati teknolojia zingine za mazungumzo zinahusisha data ya maswali yenye majibu kadhaa (predifined) kulingana na muwekaji data (developers), LaMDA ni mfumo wa teknolojia unaojifunza kupitia kusikiliza maelfu ya mazungumzo ya watu. Kupitia njia hii, kompyuta hii inauwezo wa kujibu mazungumzo ya aina yeyote kwa usahihi zaidi, na kufanya mazungumzo yawe ya kama ya wewe na rafiki yako – ambapo mnaweza kuanza mazungumzo kwa kuongelea mpira na ata kujikuta mnayamaliza mkiwa mnazungumzia masuala ya kilimo. LaMDA atakuchekesha, atakupa majibu sahihi, na anaweza pia kukubishia.
Katiba mazungumzo ambayo Injia Blake amevujisha mtandaoni, inaonekana roboti amefikia sehemu anajithamini kama mtu. Akiponda teknolojia za zamani, na akimuhakikishia muulizaji maswali ya kwamba anajipa sifa sawa na binadamu kwa sababu ana uwezo wa kuhuzunika, kukasirika, nk.
Msimamo wa Google
Google wamemsimamisha kazi injinia huyo kwa kosa la kuvujisha data za kampuni. Na msimo wao mkuu kwa jambo hili ni kwamba si kweli, leo ata miaka michache ijayo kwa mfumo huo wa AI/Akili Bandia, kufikia kiwango cha kujitambua / au kujipa sifa sawa na mwanadamu. Wanasema kinachotokea ni kuwa mfumo umekuwa bora zaidi katika kufanya mazungumzo tuu, ila si kwamba mazungumzo hayo yana maanisha mfumo umepata uelewa huru wa kifikra.
Kwa nini wana teknolojia wanaogopa suala hilo?
Kwa sasa tunatumia vifaa vya teknolojia kutusaidia kwenye jambo au kazi ambazo tayari wanadamu hatupendi sana kuzifanya. Kwenye viwanda kwa sasa kuna ukuaji wa utumiaji roboti wenye akili bandia katika kusaidia kazi za namna mbalimbali. Hofu ya wengi kwenye suala la kutengeneza kifaa cha AI/Akili Bandia chenye kuwa huru na kuwa na maoni yake ya kipekee kunaweza sababisha siku moja vifaa hivi hivi tulivyovitengeneza kutugeuka na kukataa hali wanayoweza kuiona kama ya ‘kiutumwa’. Wale wanaoangalia filamu, wanaweza kurudi kwenye filamu maarufu za The Terminator, zikihusisha miaka ambayo kutakuwa na vita kati ya wanadamu na mashine.
Unaweza kusoma mazungumzo mazima ya roboti huyo na watafiti (mazungumzo yaliyovujishwa na Injia) kupitia link hii – LaMDA interview
Soma habari zingine za Google – Kona ya Teknolojia
No Comment! Be the first one.