fbpx

Bios Cube: Majivu ya marehemu kutumika kukuza mmea

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kutana na Bios Cube! Chupa maalum ya kupandikizia mmea majivu ya marehemu na kisha kwa programu tumishi spesheli kuweza kuona maendeleo ya ukuaji wa mmea huo.

Tumezoea kuona majivu ya marehemu kutunzwa kwenye chupa maalum lakini imekuwa tofauti kwa jinsi teknolojia inavyozidi kukua.

Swali la kujiuliza ni je, inawezekana kutumia majivu ya marehemu kusaidia mmea kukua? Jibu ni ndio, inawezekana. Teknolojia mpya imegundulika huko ughaibuni ambayo itasaidia kuwaweka karibu marehemu, ni kwa kutumia kifaa kiitwacho “The Bios Incube” kilichotengenezwa na kampuni iitwayo Bios Urn.

Kifaa hicho (Bios Incube) ambacho ni nyororo, chenye mmea mweupe na kina urefu wa sm 76. Bios Incube inafanya kazi kwa ukaribu sana na Biios Urn, kitu ambacho kinaweza kuozeshwa na bakteria ikisaidiwa na programu tumishi kwenye simu janja.

Bios Incube: Kifaa ambacho chenye jukumu la kuangalia ukuaji wa mmea. Baada ya mchanganyiko kuoza majivu yanajichanganya na udongo pamoja na mizizi ya mti.

Ingawa Bios Urn imekuwepo kwa zaidi ya miaka miwili sasa lakini Bios Incube ni bidhaa mpya ambayo imeundwa kwa wale wanaotaka kuwa karibu zaidi na mpendwa wao. Bios Urn ni ndogo, ina umbo la “cylinder” likiwa na majivu ya marehemu, mchanga pamoja halafu mbegu juu yake.

majivu

Bios Urn inaundwa na karatasi, Hewa ya ukaa (Carbon) na Cellulose.

Ukingo wa juu wa Bios Incube unatenganishwa na uzio na kufanya udongo kujitengenga na Bios Incube. Uzio huo ambao pia ni pipa la maji lenye uwezo wa kuhifadhi maji mpaka lita 11.4. Kwa maelezo zaidi tazama picha jongefu hapo chini.

INAYOHUSIANA  Google kuendelea kushirikiana na Huawei kwa siku 90 zijazo

Unaizungumziaje teknolojia hii ambayo inalenga kuwa karibu kabisa na yule ambayo hayupo tena duniani? Tuandikie maoni yako kuhusu makala hii. Siku zote TeknoKona tunajali.

Vyanzo: Big Think, live science

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|