fbpx
Android, Microsoft, Teknolojia, Windows

Bill Gates: Kosa kubwa la muda wote ni kuiacha Android kuongoza

bill-gates-kosa-kubwa-la-muda-wote-ni-kuiacha-android-kuongoza
Sambaza

Katika mahojiano ya hivi karibuni, mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft, Bill Gates amenukuliwa akisema kuwa katika moja ya kosa lake kubwa la wakati wote alilolifanya ni kuiacha Android kuongoza katika mifumo ya uendeshaji Duniani.

Bill Gates
Bill Gates.

Amesema katika ulimwengu wa programu anayeongoza katika kuwa na programu endeshaji inayotumika kwenye vifaa vingi zaidi ndiye anakuwa mshindi wa masoko yote. Hivyo kwa upande wa Microsoft imefanya kosa kubwa ambalo limeifanya Android kuongoza sokoni.

INAYOHUSIANA  AppStar Kutoka Vodacom, Watengenezaji wa Apps Mpo?

Android kwa sasa ndio mfumo endeshi unaoongoza kwa kutumiwa na watu wengi zaidi duniani ukifuatiwa na mfumo wa Microsoft, yaani Windows.

Microsoft ilijaribu kuleta programu endeshaji spesheli kwa ajili ya simu iliyokwenda kwa jina la Windows Mobile kwa upande wa simu zake za Windows Phone lakini haikupokelewa vizuri sokoni na pia kwa watengenezaji wa apps. Microsoft ikajikuta bado inabaki ikitamba katika kompyuta zaidi.

android google
Ukuaji wa nafasi ya Android kwenye simu zinazotumika ukilinganisha na programu endeshaji zingine (Mwaka 2009 hadi 2016)

Kwa sasa Android inatumika katika 85% ya simu janja zote duniani.

INAYOHUSIANA  Fanya Kompyuta Yako Iweze Rusha WiFi Kwa Vifaa Vingine!

Google walinunua kampuni ya iliyokuwa inatengeneza programu endeshaji ya Android mwaka 2005 kwa dola milioni 50 mwaka 2005 hii ikiwa ni miaka miwili nyuma kabla ya Apple kuja na iPhone mwaka 2007, na simu ya kwanza inayotumia Android iliingia sokoni mwaka mmoja baada ya iPhone – mwaka 2008.

Apple kupitia iOS na Google kupitia Android walibadilisha kabisa mtazamo wa biashara za simu, na apps – makampuni kama vile Microsoft, Nokia na BlackBerry walichelewa kubadilika na hii hivyo kujikuta nyuma kimaendeleo katika sekta hii.

INAYOHUSIANA  Apple Yazidiwa Na Android Huko Nchini India!

Microsoft ishakata tamaa katika soko la programu endeshaji ya simu, tayari washatuma ujumbe kwa watumiaji wake wa simu za Windows 10 Mobile ya kwamba kufikia Disemba mwaka huu hawataweza kupata masasisho tena ya programu endeshaji yao na hivyo waamie kwenye simu za Android au iOS.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.