fbpx

WhatsApp, Facebook na Instagram zapata shida: Fahamu maeneo yaliyoathirika

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Hadi sasa kama ni mtu wa mitandao ya kijamii basi utakuwa umekwishaona taarifa ya kwamba apps za WhatsApp, Facebook na Instagram zapata shida inayosababisha mamilioni ya watumiaji wake kushindwa kupata huduma iliyo bora kwa sasa.

Watumiaji walioathirika wameshindwa kudownload picha, video n.k hasa kwenye jumbe za WhatsApp ila ata wa Instagram na Facebook wamepata shida hiyo hiyo.

WhatsApp, Facebook na Instagram zapata shida

Mamilioni ya watumiaji wameathirika

Nini kimesababisha;

Tatizo limetokea kwenye baadhi ya kompyuta mama za data (Servers) zinazomilikiwa na Facebook ambazo zinahudumia huduma hizi zote tatu.

INAYOHUSIANA  Uber: Makosa matano yanayoweza kukusababishia usipewe huduma tena

Maeneo yaliyoathirika;

Kwa Tanzania tatizo lipo ingawa si ukubwa sana; ila tayari wapo ambao wanaathirika, tatizo kubwa limekuwa barani Ulaya na Amerika ya Kusini. Mitandao inayohusisha huduma za kutambua okosekaji wa huduma za kimitandao imeweza kutoa data ambazo zinaonesha mataifa yaliyoathirika zaidi;

Angalia picha hii, kwenye wekundu zaidi ndio kwenye shida zaidi kwa wingi wa watumiaji ambao wameshindwa kupata huduma za apps hizi kwa sasa.

Facebook na Instagram zapata shida

WhatsApp, Facebook na Instagram zapata shida: Maeneo yaliyoathirika

Hii si mara ya kwanza na kwa huduma za kimtandao ni jambo ambalo hutokea, ila kwa Facebook inawezekana ikawa ni muda wa kujitazama na kufanya maamuzi ya kuboreshwa kwani ni mwezi wa tatu tuu huduma hizo tatu zilipitia matatizo haya haya. Na kwa kila dakika ambayo huduma hizi zinakuwa zinapata shida kampuni hiyo hupoteza mapato mengi kutokana na kushindwa kurusha huduma ya matangazo.

INAYOHUSIANA  SIGNAL: Facebook Waja Na Kipengele Kipya Kinachosaidia Waandishi Wa Habari!

Soma habari mbalimbali kuhusu apps mbalimbali -> Teknokona/Apps

Vyanzo: India Today na vyanzo mbalimbali
Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.