Kama umekaa karibu na watoto utagundua kuwa wanapenda sana Youtube. Wanapenda sana kuangalia video kwenye mtandao huo ingawa Youtube ni kwa ajili ya watu kuanzia miaka 13 na kuendelea. Sasa hili lishatokea watoto chini ya miaka 13 bado wanaangalia video hizo za Youtube, hapo ndipo Google inapokuja na Youtube Kids!
App hii mpya inatarajia kutolewa rasmi februari 23 na litakua ndio toleo la kwanza la Google ambalo linamuangalia mtoto kwa macho mawili.
YAFUATAYO NI MAMBO YANAYOPATIKANA KATIKA APP
VIpengele Vichache Vya Chaneli Na Hakuna Comment
Youtube ya kawaida ina makundi mengi ya chaneli lakini katika Youtube kids kuna makundi manne tuu: Muziki, Michezo ya Maigizo, Elimu na Kuchunguza (Explore) Zile Video Bora. Na pia kingine kikubwa ni kwamba Youtube Kids haina kipengele cha Comments. Hii inamaanisha mtoto hataweza kusoma wala kuandika ‘comment’ akiwa ndani ya Youtube kids.
Toleo la kwanza: Kwenye simu janja
Watoto wengi sasa wanatumia simu janja na tablets na sio kompyuta tena. Ndio wanapenda sana simu na hii ndio sababu kubwa youtube kids kwanza itakuja katika simu tuu. Itaanza na toleo la Android kwanza itakapotoka (februari 23). Ni vizuri pia kutegemea toleo la iOs hapo mbeleni
App Inadumisha Malezi Ya Mtoto
Wazazi wanaweza fanya juu chini ili kudhibiti matumizi ya Youtube kwa watoto wao kuwa ya kupindukia. Mzazi anaweza Amuru App Hiyo mda wa kutumika na kuacha kutumika na kisha kuweka neno lake la siri. Mda wa kutumika ukiisha inabidi mtu aweke neno siri la mzazi ili kufungua tena App hiyo. Hata hivyo hiyo App Ita ‘Sensi automatikali’ maneno kama vile ‘sex’ na kumlazimu mtoto aweke (aandike) neno lingine tofauti.
Youtube kids itakuwa na matangazo pale itakapo achiwa, lakini matangazo ya biashara yataendana na Sera ya Youtube ili kuwa na uhakika kwamba yataendana na hadhira (Watoto). App haitaunganishwa na Akaunti za Google (Akanti Moja, Google Nzima) kwa hiyo taarifa zote za watoto hazitakusanywa na kuhifadhiwa.
SOMA PIA: Twitter Imeachia App Mpya Ya VineKids Kwa Ajili Ya Watoto!
No Comment! Be the first one.