Wikipedia imetimiza miaka kumi na tano tangu kuanzishwa kwake na kama ulikua hujui basi ukurasa wa George Bush aliyekuwa raisi wa Marekani ndio unaoongoza kwa kuwa na marekebisho mengi zaidi. Wikipedia ni ukurasa wa unaolenga kuhakikisha kwamba taarifa zinapatikana kwa wote.
Wikipedia tofauti na encyclopedia nyingine za mtandaoni inaruhusu mtu yeyote kuweza kufanya mabadiliko ya makala zake na taarifa nyingine. Mfumo huu ndio hasa umechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa wikipedia hasa ukizingatia kuwa imekuwa na waandishi na warekebishaji wengi.
Katika kusherekea miaka 15 tangu kuanzishwa kwake Wikipedia wametoa orodha ya makala zilizofanyiwa marekebisho mengi zaidi. Bush ameongoza orodha hiyo akiwa na marekebisho 45,862 akiwa ameongoza kwa tofauti ya marekebisho karibu 3000 dhidi ya ukurasa wa WWE. Katika mtiriliko huo kurasa za Marekani, Wikipedia wenyewe, Yesu pamoja na Kanisa Katoliki pia zilipata marekebisho mengi zaidi.
Toka ilipoanzishwa wikipedia ina makala zaidi ya 36 milioni na huku ikiwa na wachangiaji zaidi ya 80000 ambao wanafanya kazi ya kujitolea. Changamoto kubwa zaidi wanayopata Wikipedia ni kushuka kwa idadi ya wachangiaji ambayo inadaiwa ni kutokana na sheria ngumu ambazo Wikipedia inaweka dhidi ya wachangiaji wake.
soma zaidi kuhusu makala miaka 15 ya Wikipedia hapa
No Comment! Be the first one.