fbpx

Uwezo wa kuteua watu wa kurekebisha taarifa kwenye WhatApp

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

WhatsApp imekuwa mstari wa mbele kuleta vitu vya kuvutia kwenye programu tumishi maarufu zaidi duniani kwa kurahisisha mawasiliano na sasa wameleta kitu kizuri kwa wale ambao wanachukizwa na kubadilishwabadilishwa taarifa za kundi.

Kwenye WhatsApp katika kipengele cha kundi ni jambo la kawaida sana kwa mtu yeyote yule kuweza kubadilisha jina la kundi/kichwa cha habari au pichab kwenye kundi husika lakini kitendo hicho sasa kipo njiani kukoma kwani katika sasisho lijalo la kwenye WhatsApp; kiongozi wa kundi ana uwezo wa kuruhusu mtu yeyote yule kubadilsha jina la kundi/picha au kuruhusu baadhi ya watu tu ndio waweze kurekebisha taarifa mbalimbali za kwenye kundi husika.

Sasa wewe kama kiongozi wa kundi kwenye WhatsApp inabdi uingie Group info > Group settings > Edit group info ili kuweza kuamua kile ambacho utapenda kundi unaloliongoza lisiwe na uwezo wa kubadilisha taarifa (picha/maelezo) kadri wapendavyo.

uwezo wa kuteua watu wa kurekebisha taarifa

Sasisho jipya la kwenye WhatsApp ambalo linampa nguvu kiongozi wa kundi husika kuweza kuamua nani na nani wanatakuwa na uwezo wa kuweka vichwa vya habari vipya au kubadilisha picha kama alama ya kundi.

Kwa wale wote wanaotumia WhatsApp ya majaribio, BETA kwenye Android kuanzia toleo la 2.18.132 watakuwa wameshaona sasisho hili jipya. Kwa wanaotumia iPhone na simu za Windows pia wamepokea sasisho hilo.

Masasisho mengine yanatarahiwa kuletwa kwenye programu tumishi yenye watumiaji zaidi ya watu bilioni moja. Moja ya vitu hivyo ni kiongozi wa kundi kuzuia kila mtu kwenye kundi kuweza kutuma chochote au kuteua baadhi tu ya watu kuweza kuwasiliana kwenye kundi husika.

Vyanzo: Gadgets 360, WABetaInfo

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Miaka 30 ya mafaili ya mtindo wa GIF. - Fahamu historia yake!
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.