fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Android Apple

Wakati iWatch Inasubiriwa, Wachina Waja Na iWatch Feki Za Android!

Wakati iWatch Inasubiriwa, Wachina Waja Na iWatch Feki Za Android!

Spread the love

Fitness-Workout-apps-Apple-WatchSaa Janja (Smart Watch) ambazo zinachukua muonekano (design) kama ule wa saa za Apple maarufu kama iWatch zimeanza onekana katika masoko ya kimtandao (online shops)  mbalimbali huko nchini china.

Picha za simu za Apple ambazo zinauzwa kwenye masoko hayo hazi jaandikwa neno ‘Apple Watch’ bali tunda la epo limewekwa badala ya neno ‘Apple’  na kufuatiwa na neno ‘watch’.

Kutokana na kwamba iWatch zimetangazwa na kuongelewa sana kwenye mtandao, hali hii imefanya watu wengi na wateja kwa ujumla kujua au kuwa na wazo kuwa itakua na muonekano upi. Mambo yote haya yamewafanya watu kujua jinsi ilivyo ki undani zaidi na vipengele vyake. Hii pia imesaidia watu kuweza kutofautisha saa janja ya Apple katika saa janja zingine

SOMA PIA: iWatch: Apple Na Saa Ya Milioni 18+

Licha Ya Kwamba iWatch inakaribia kuingia sokoni rasmi baadhi ya wafanya biashara wakubwa wamechukulia hii kama ni fursa. Wametoa na kuuza saa zao ambazo ni feki huko china, Ndio kabisaaaaa! Saa hizi ni bei rahisi sana kulinganisha na bei ya saa orijino kutoka Apple

SOMA PIA  Ifahamu Simu ya Tecno R6 LTE! #Uchambuzi

Mfano mzuri ni kwenye soko la kimtandao la kimataifa la Alibaba. Mtandao wa  Taobao (www.Taobao.com) ambao umeweka bidhaa kama AW08 na iWatch katika mtandao huo.  Badala ya saa hizi kuwa na ‘Apple watch OS’ cha kushangaza Taobao wameweka ‘Apple Watch’ za kwao kwa kuwa zina zinatumia mfumo wa Android wa google

taobao

Mtandao wa Taobao (www.Taobao.com) Ukionyesha Bidhaa Zake (iWatch Feki)

Wachina ni Watumiaji wazuri wa bidhaa za Apple na pengine labda wanataka kuwa wa kwanza kuonja ladha ya Apple iWatch mikononi mwao. La muhimu kuangalia hapa ni kitu wanachonunua kama ni feki au orijino, sawa kwa sasa iwatch zinazouzwa ni feki tuu kwa sababu bado haijaachiwa rasmi na Apple, vipi zikitoka?

Kuwa Wa Kwanza Kusambaza Makala Hii Na Kuungana Nasi Katika Kurasa Zetu Za Twitter, Facebook Na Instagram

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Comments

  1. GabrielMathewAlaMgongolo - March 24, 2015 at 17:05 - Reply

    Samahani nipo nje ya maada kidogo naulizia applications itakayo niwezesha kuperuzi website ambazo zipo recommend kwa baadhi ya nchi.

  2. GabrielMathewAlaMgongolo inawezekana soma hapa -> http://teknokona.com/2014/11/26/hola-fungua-mitandao-inayozuiwa-kufunguka-tanzania/

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania