Biashara ya magari yanayojiendesha yenyewe imeonekana kuivutia kampuni nguli ya Apple katika biashara hiyo; Google, Tesla ni baadhi ya makampuni yanayojihusisha na teknolojia ya magari yanayojiendesha yenyewe.
Kampuni ya Apple imetangaza mipango yake ya kuunda magari yanayojiendesha. Kampuni hiyo imekiri hayo kwa mara ya kwanza kwenye barua kwa wasimamizi wa uchukuzi Marekani.
Apple inafurahishwa sana na uwezo wa mifumo ya kutumia kompyuta kwenye maeneo mengi, ikiwemo uchukuzi. Apple wanaamini kwamba kuna manufaa mengi ambayo yatapatikana kijamii kutoka kwa magari yanayojiendesha.
Hata hivyo, kampuni ya Ford, ambayo pia ina mipango ya kuunda magari kama hayo, ambayo inadhamiria yataweza kutumiwa barabarani mwaka 2021 na inaendelea na mpango wake ikifahamu kwamba Apple nao wanaunda magari kama hayo.
Soma pia: Uhusiano kati ya Tesla na Apple katika teknolojia ya magari
Mwezi Oktoba, kampuni inayounda magari yanayotumia umeme, Tesla, ilitangaza kwamba magari yake yote sasa yataundwa yakiwa na programu ya kuyawezesha kujiendesha bila kuwa na dereva.
Tayari Apple imesajili anwani za tovuti mtandaoni ambazo zinahusiana na magari, zikiwemo apple.car na apple.auto. Ni matumani yetu sote tumekaa ‘mkao wa kula’ kusubiri kuona kama Apple watafanya vyema katika biashara ya magari yanayojiendesha yenyewe.
Vyanzo: BBc, mitandao kadha wa kadha.