Unakumbuka makala kuhusu app ya Facebook kutumia chaji nyingi kwenye simu yako ata kama hauitumii? Basi kutana na app ya Metal, app kwa ajili ya Facebook isiyotumia chaji sana katika kufanya kazi.
Ingawa app rasmi ya Facebook ni moja ya app zinazofanyiwa maboresho kwa kasi zaidi, bado app yao ni moja ya app inayotumia kiwango kikubwa zaidi cha chaji katika simu ya Android ukilinganisha na app zingine.
Masasisho (updates) ya Facebook app kwa ajili ya Android hufanyika kila baada ya wiki mbili
Kutokana na hili ndio wazo la ujio wa app hii inayofahamika kwa jina la Metal likaja. App ya Metal inamsaidia mtu kuingia katika huduma ya Facebook na Twitter bila uhitaji wa wewe kupakua apps zake spesheli. Na sifa kubwa kabisa waliyonayo ni utumiaji mdogo kabisa wa chaji unaofanywa na app hiyo katika ufanyaji kazi wake.
Na app hiyo ni ndogo sana kiukubwa, takribani MB 1.4 tuu kwa faili lake la kupakulia (install) – APK.
Wakati app ya Facebook na Messenger zinauweza kuchukua takribani nafasi ya MB 300 katika simu yako…app hii inatumia takribani MB 6-12 kutegemea na matumizi yako.
App hiyo iliyofanyiwa ubunifu kwa kutumia ‘Material design’ (sheria ya ubunifu kutoka Google) imekwisha jizoelea umaarufu sana kwa wachunguzi mbalimbali.
Kwa kutumia muonekano wa toleo la mtandao wa Facebook la kawaida wameweza kutengeneza app inayoboresha muonekano na utumiaji wa huduma ya Facebook moja kwa moja kama vile app nyingine yeyote.
Kupitia app hii pia kunakuwa hakuna ulazima wa kutumia app ya Facebook Messenger ilikukuwezesha kuchat/kutuma ujumbe. Unaweza kusoma na kujibu ujumbe ndani ya Facebook bila ulazima wa kutumia app ya Messenger (ambayo nayo inasifa ya utumiaji mkubwa wa chaji).
Download – Google Play | Metal
Soma Pia – App ya Facebook, Inakula chaji 20% zaidi na Inafanya Simu yako kuwa Nzito!