fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps whatsapp

Sasa unaweza Kutuma na Kupokea Documents katika WhatsApp

Sasa unaweza Kutuma na Kupokea Documents katika WhatsApp

Spread the love

WhatsApp sasa imeanza kuruhusu watumiaji wake kutumiana documents, katika toleo lake lililotoka Jumatano asubuhi kumeongezwa uwezo wa kutuma na kupokea mafaili ya PDF.

Wapinzani wakubwa wa mtandao huu kama vile Telegram wamekuwa na huduma hii kwa muda mrefu na pengine hii ni hatua ya makusudi kutoka kwa WhatsApp kupambana na wapinzani.

Mabadiliko haya yanakuja na update iliyotoka mapema Jumatano, kama haujaanza kuona huduma hii mpya basi unatakiwa ku-update app yako. Mabadiliko haya yamekuja kwa pamoja kwa watumiaji wa iOS pamoja na Android (Ha!ha! mambo ya haki sawa), na pamoja na kuongezwa huduma ya kusambaza mafaili pia kuna mabadiliko machache kwenye muonekano wa WhatsApp.

documents

Muonekano mpya wa Whatsapp Kutuma na Kupokea Documents katika WhatsApp

Kupata Mabadiliko haya ni lazima kupakua toleo jipya la WhatsApp ambalo tayari lipo katika soko la app la playstore, ama kama kwa namna moja ama nyingine playstore haikupi toleo jipya zaidi la WhatsApp basi unaweza kupakua toleo la app hii la APK ambalo linapatikana HAPA (Soma kwanza jinsi ya ku install app kwa katika mfumo wa APK ).

WhatsApp-iOS-App-can-share-documents

Muonekano mpya wa WhatsApp for iOS

Baada ya kuwaumeisha shusha na kuinstall toleo jipya zaidi la WhatsApp yako ukiifungua na kwenda sehemu ya kuambatanisha media (pale ambapo huwa tunaenda kwaajiri ya kuambatanisha picha ama muziki) kisha unatakapofungua utaona kuna vipengele sita (Ndio hata kabla ya update vilikua vipengele sita ila ni kwamba sasa hivi kipengele cha video na photo vimeunganishwa na kutengeneza kipengele kimoja cha camera) ambapo kimoja kimeandikwa documents hiki ndicho hasa ambacho kimeongezwa kwaajiri ya kusambaza mafaili.

documents katika whatsapp

Muonekano wa mafaili uliyoyasambaza

Kwa sasa ni aina  moja tu ya mafaili ambayo inaungwa mkono na WhatsApp hii ni aina ya PDF, ni matumaini kwamba matoleo yanayokuja ya WhatsApp yatakuwa yanaunga mkono aina nyingine za mafaili kama  vile .doc.

SOMA PIA  Instagram Lite Sasa Yaanza Kupatikana.

Huu ni mwanzo mzuri kwa WhatsApp kujiimarisha kama app ambayo inatumiwa na watu kwa matumizi zaidi ya kijamii.

Je umekwisha anza kutumia toleo hili jipya la WhatsApp? je unalionaje? tuandikie maoni yako.

Comment

Comments

  1. […] hivi karibuni tuu WhatsApp walileta uwezo wa kutumiana mafaili ya mfumo documents – PDF n.k, na pia wakaleta app yao kwenye kompyuta kupitia programu spesheli za kupakuliwa kwenye kompyuta za […]

TeknoKona Teknolojia Tanzania