fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps Facebook Maujanja Mtandao wa Kijamii

Namna ya kuzima Video zinazocheza zenyewe Facebook katika simu na Kompyuta

Namna ya kuzima Video zinazocheza zenyewe Facebook katika simu na Kompyuta

Spread the love

Baadhi ya wasomaji wetu moja ya swali walilouliza ni kutaka kujua namna ya kuzuia video zinazocheza zenyewe (automatically) katika App ya Facebook katika simu zao.

Tumeona ni vyema kuandaa somo fupi kwa ajili ya maslahi ya wengi ambao wanausumbufu kama huo lakini hawakupata nafasi ya kuuliza.

Ni kweli Video zinapocheza zenyewe hupelekea kula Data zako bila ya sababu ya msingi kwa kucheza video ambazo hukukusudia.

Leo tunakuonesha namna ya kuzima video kucheza zenyewe Facebook katika Simu Janja na katika Kompyuta.

Kuzima Video zinazocheza zenyewe Facebook:

Tuanze kwa njia ya simu.

1. Unatakiwa kufungua App yako ya Facebook.

2. Angalia juu upande wa kulia, utaona mistari mitatu na ubonyeze hapo.

SOMA PIA  Utafiti: Mitandao ya kijamii chanzo cha habari kikubwa kwa watu wengi

3. Utafungua ukurasa wenye menu kadhaa, fungua ‘App settings’.

4. Bonyeza ‘Auto-play’.

5. Chagua Never ‘Auto-play Videos’.   kuzima Video zinazocheza zenyewe Facebook Kwa njia ya Kompyuta fuata hatua zifuatazo;

1. Fungua programu ya ‘facebook’.

2. Angalia juu upande wa kulia uatona alama kama ya mshale ulioelekea chini, bonyeza.

SOMA PIA  Google I/O - Apps za Android ktk Chrome OS, Toleo la Android 7 na habari nyingine!

3. Itafungua Menu bonyeza palipoandikwa ‘Settings’.

4. Angalia upande wa kushoto chini fungua palipoandikwa ‘Videos’.

5. Angalia ‘Auto-play Video’ upande wa kulia bonyeza.

6. Chagua ‘Off’.

Bila shaka utakuwa umefanikiwa kuzima Video zinazocheza zenyewe. Kama una maoni au swali usisite kutuandikia kupitia hapo chini sehemu ya maoni.

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania