Dunia ya leo ina mengi mazuri ambayo hayakuwepo huko miaka ya nyuma. Biashara kwa njia ya kidijitali imekuwa na kuingizia kipato kikubwa makampuni makubwa kama Amazon ambayo sasa inataka kuja na mpango wa nunua sasa lipa baadae.
Amazon imeajiri wafanyakazi wengi ambao wanafanya kazi ya kuandaa bidhaa za wateja kisha kuzituma/kuwapelekea mpaka walipo. Lakini ubunifu kwenye biashara ni kitu muhimu sana ambapo sasa Amazon itaweza kuuza bidhaa halafu wateja wakalipa baadae.
Hivi karibuni Amazon imeingia makubaliano ya kibiashara na Affirm (kampuni) ambapo wawili hao watafanya kazi kwa kushirikiana na kuhakikisha mteja anaweza akanunua bidhaa na kulipa baadae (kulipa kidogo kidogo). Wakati wa kukamilisha kufanya manunuzi ni lazima mteja akubali kipengele cha kuangalia historia yake ya kufanya miamala.
Amazon imeingia makubaliano ya kushirikiana na Affirm ambapo iwapo mteja atachagua kulipa kwa mfuo huo hakutakuwa na makato yaliyojificha ama kupigwa faini kwa sababu ya kuchelewa kufanya malipo.
Mpango huo wa “Nunua sasa lipa baadae” ambao Amazon inaufanyia kazi kuuleta kwa wateja utaruhusu mtu kuweza kununua kitu cha kuanzia $50 au zaidi na kulipa kidogo kidogo kila mwezi. Hata hivyo, huduma hiyo haitahususisha bidhaa kama chakula, sinema, vitabu.
Tayari huduma hiyo imeshawekwa kwenye majaribio kwa watu wachache lakini ni ngumu kusema iwapo imevutia watu ama la! Na haijawekwa wazi lini itaanza kupatikana kwa wote.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
No Comment! Be the first one.