fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Facebook Mtandao wa Kijamii Teknolojia

Jinsi ya kufuta Akaunti yako ya Facebook

Jinsi ya kufuta Akaunti yako ya Facebook
Spread the love

Je ungependa kufuta akaunti yako ya Facebook? Kama unatumia mtandao wa kijamii wa Facebook na umechoka kuutumia mtandao huo au unataka ufute taarifa zako za huko na kuanza upya basi unaweza kufanya hivyo kwa kufuata hatua zifuatazo:

  1. Ingia kwenye menyu yako ya Facebook iliyopo juu kwenye kona ya kulia.  kufuta akaunti yako ya Facebook
  2. Ukiwa kwenye hiyo menyu shuka chini mpaka uone sehemu imeandikwa Settings & privacy. kufuta akaunti yako ya Facebook 
  3. Baada ya hapo ingia kwenye sehemu iliyoandikwa Settings.  kufuta akaunti yako ya Facebook
  4. Ndani ya settings ingia kwenye sehemu ya kwanza ambayo itakuwa imeandikwa Personal and account information.  kufuta akaunti yako ya Facebook
  5. Shuka mpaka kwenye chaguo la mwisho lililoandikwa Account ownership and control.  kufuta akaunti yako ya Facebook
  6. Ukiwa humo utaona sehemu iliyoandikwa Deactivation and deletion, chagua hii  kufuta akaunti yako ya Facebook
  7. Baada ya hapo utaulizwa kama unataka kuizima account yako ya Facebook kwa muda au unataka kuifuta kabisa account yako, Hapa utachagua inayokufaa kisha utatakiwa kuingiza nywila yako.
SOMA PIA  Ifanye app ya WhatsApp isichukue nafasi kubwa kwenye simu yako

Angalizo: Akaunti ya Facebook hufungwa siku 30 baada ya kutuma maombi ya account yako kufungwa.

Endelea kutembelea tovuti yetu ili uweze kupata maujanja zaidi katika matumizi ya huduma za mtandaoni. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kufuta akaunti yako ya Facebook soma hapa.  Soma makala zetu nyingine zinazohusu mitandao ya kijamii hapa.

Semu Msongole

Digital Marketing Strategist, Content Writer, and Social Media Manager at Teknokona Blog.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania