Chip imegunduliwa na mwanasayansi mmoja yenye ukubwa wa ukucha ambayo itabadilisha historia nzima ya betri na uchajishaji wa betri ndogo na kubwa kwa kupunguza muda wa kuchaji hadi walau dakika kumi.
Betri ni kitendawili ambacho bado hakijapata ufumbuzi tangu simu janja zilipovumbuliwa, makampuni yamekuwa yakihangaika kufanya ubunifu utakao weza kutupa betri yenye kukaa na chaji mda mrefu.
Hii siyo mara ya kwanza kwa wanasayansi kujaribu kutatua tatizo la betri na chaji katika smartphone, mwezi uliopita tuliandika hapa juu ya Huawei kuja na betri inayochaji haraka zaidi tofauti ni kwamba huawei wao wametengeneza betri ambayo inaundwa na anode yenye uwezo wa kupitisha umeme kwa haraka zaidi lakini hii chip yenyewe itaisaidia charger ya simu kujua tabia za betri hivyo kuchunga umeme unaoenda katika betri.
Chip hii iliyogunduliwa na profesa Rachid Yazami wa chuo kikuu cha teknolojia cha Nanyang ina ukubwa kama wa ukucha, chip hii inauwezo wa kuangalia ukubwa wa betri na hali ya chaji katika betri katika wakati husika. Chip hii huweza kupunguza au kuongeza umeme unaoenda katika betri kutokana na hali ya betri katika wakati husika hivyo huupunguza saana muda wa kuchaji betri hadi walau dakika 10.
Chaja za siku hizi hazizingatii hali ya betri husika katika muda husika bali zenyewe hupeleka umeme katika kiwango kile kile mwazo hadi mwisho, hii husababisha betri kuchukua muda mrefu kujaa chaji na pia wakati mwingine husababisha betri kuharibika haraka.
Kama chip hii kweli itafikia hatua za uzalishaji basi tutegemee saana utabadili historia ya mifumo ya simu janja, na pia simu zitakazotengenezwa zitakuwa na mambo mengi ambayo kwa sasa hayawezekani kwa kuwa tunahitaji kutunza chaji za simu zetu.
Makampuni yote ya nayohusika na utengenezaji wa simu janja kwa sasa yanaangalia namna nzuri ya kushughulikia hili tatizo la kudumu kwa chaji katika simu, pengine hii ni moja kati ya mabo ambayo bado hayajapata ufumbuzi wa kudumu.
Endelea kufuatilia mitandao yetu ya kijamii kwa taarifa zaidi za kiteknolojia kwa kiswahili pindi zinapotokea, tufate twitter instagram na facebook
One Comment