Imeripotiwa kwamba mtandao maarufu wa Instagram unayafanyia majaribio mabadiliko ambayo yataruhusu kwa mtumiaji mmoja kuweza kutumia zaidi ya akaunti moja . Instagram itakuwa imefuata nyayo za mitandao mingine mikubwa ya Twitter na Facebook ambayo inamruhusu mtumiaji mmoja kuweza kumiliki akaunti zaidi ya moja.
Instagram hairuhusu akaunti zaidi ya mmoja kwa mtuniaji mmoja hivyo kama unataka kutumia akaunti nyingine basi inakubidi kutoka na kuingia kwa akaunti unayoitaka, wakati kwa twitter kama una akaunti zaidi ya moja unaweza kuzihudumu bila ya shida yeyote ile unachofanya ni kuchagua tu akaunti gani unaitaka.
Kama majaribio haya yakifanikiwa na kuanza kutumika basi hii itawaruhusu watumiaji wa instagram kuweza kutumia akaunti nyingi kwa mtumiaji mmoja, hii itawasaidia saana watu wanaofanya kazi za social media management ambao mara nyingi huwa na wateja wengi ambao wote wana akaunti tofauti za instagram na unatakiwa uweke post na kujibu comments.
Mtandao wa The verge umeripoti pia habari hii na kusema kwamba insta wanafanya majaribio yatakayo weza kuwaruhusu watumiaji wake kuwa na akaunti zaidi ya moja. Hii inatokana na ukweli kwamba hivi karibuni insta walitangaza kubadilisha sera zao juu ya watengenezaji wa third party app, hii inaonesha kwamba insta wanataka kuhakikisha kwamba kila kitu wanakifanya wao.
Pengine Instagram wakifanya haya mabadiliko watu wengi zaidi watajikita katika ku-manage akaunti za biashara, nawe msomaji pengine hii ndio nafasi yako yakupata ajira. Angalia bishara zinazokuzunguka chagua ambazo zinaweza kupata wateja katika mtandao kisha ongea na mmiliki wa biashara na umshauri kufungulia akaunti ya instagram utakayo msaidia kuitunza ili aweze kupata wateja wengi mtandaoni kwa malipo kidogo kwako.
Instagram ni mtandao unaopendwa saana hapa bongo, kama vile ilivyo kwa mtandao wa Facebook na huduma ya kuchati ya WhatsApp. Instagram ina watumiaji wengi sana Tanzania hivyo imefanikiwa kufungua fursa hadi za kibiashara. Na hivyo uwezo huu utapendwa sana na watu wanaotumia simu moja kwa kusimamia akaunti kadhaa za kibiashara .
Endelea kufuatilia habari mbalimbali katika mitandao yetu ya twitter, facebook na Instagram
One Comment