fbpx
Saa

Nubia Alpha: Simu janja inayovaliwa mkononi

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

Sambaza

Kwa namna yake teknolojia ya simu zinazojikunja zinarudi kwenye ushindani/machoni pa watu. Kama utakuwa ni mpekuzi mzuri kuhusu teknolojia utafahamu kuwa makampuni mbalimbali yana buni vifaa vya kidijiti vinavyokunjika mathalani simu janja inayovaliwa mkononi.

Wengi wetu siku hizi tunafahamu kuwa kuna saa janja ambazo zina uwezo wa kufanya mambo mengi tuu pamoja na kuweza kupiga.kupokea simu, kutuma ujmbe mfupi wa maneno, n.k lakini hata kufuatilia miendendo ya miili yetu kiafya zaidi.

Siku kadhaa zilizopita ulimwengu ulipata kufahamu kwa taarifa rasmi kabisa kuhusu “Simu janja inayovaliwa mkononi” au kwa jina rahisi Nubia Alpha. Ni saa janja kama nyinginezo ambazo tunazifahamu pamoja na sifa zake lakini kwa Nubia Alpha tutaangazia zaidi upande wa simu janja:

>Muonekano/Kipuri mama

Kioo ni cha OLED urefu wa ni inchi 4 tu ambacho ni cha mguso; ili kuweza kufikia programu zilizowekwa inambidi mtumiaji aguse kidogo kwenye kioo kwenda kulia-kushoto. Upnde wa kipuri mama kama kiongozi wa shughuli zote ni Snapdragon Wear 2100.

>RAM/Diski uhifadhi

Nubia Alpha kama saa janja nyingine zinazotolewa na makampuni mengi tuu ambayo yanatengeza bidhaa hiyo kwenye RAM wanaweka GB 1. Kwenye upande wa memori ya ndani saa janja hii ina GB 8 pekee.

Simu janja inayovaliwa mkononi

Nubia Alpha-Simu janja inayovaliwa mkononi.

>Kamera/Betri

Zile picha za kujipiga mwenyewe inawezekana kabisa kwa kamera ya MP 5. Betri yake ina 500mAh ambapo kwa mujibu wa walioitengeneza ina uwezo wa kudumu na chaji kati ya siku moja hadi mbili.

INAYOHUSIANA  Ushirikiano kati ya HaloPesa na VISA wazinduliwa

>Bei/Mengineyo

Bei ya Nubia Alpha ipo katika makundi matatu; kundi la kwanza ni zile ambazo zinatumia Bluetooth (unaweza ukaunganisha na simu kuweza kupiga/kupokea simu, kutuma SMS, kutuma/kupokea kitu kutoka kifaa kingine) zinauzwa $510|zaidi ya Tsh. 1,173,000. Kundi la pili ni zile ambazo zinatumia eSIM ambazo ni $624|zaidi ya Tsh. 1,435,200. Kundi la tatu na la mwisho ni zile za rangi ya Dhahabu-$737|zaidi ya Tsh. 1,695,100.

Nubia Alpha ina uwezo wa kufuatilia mapigo ya moyo, ukakamavu wako wakati wa mazozezi, kufanya malipo kwa njia ya QR Code-AliPay, kuunganisha na spika za nje kwa njia ya Bluetooth. Inawezekana kutumia sauti kuweza kuandika ujumbe badala ya kicharazio.

Simu janja inayovaliwa mkononi

Nubia Alpha ya rangi ya Dhahabu ndio itakayokuwa inauzwa kwa bei ya juu zaidi kuliko nyingine.

Nubia Alpha inatumia mfumi endeshi wa Android pia inauwezo wa kukunjwa hadi mara laki moja bila shida yoyote na zitaanza kupatukana kuanzia mwezi Aprili.

Vyanzo: The Verge, GSMArena

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.