Katika onyesho ambalo hufanyika mara moja kila mwaka (MWC19) likikutanisha makampuni mbalimbali sehemu moja kila mmoja kwa muda wake akatambulisha bidhaa alizonazo, Xiaomi wakatoa Mi Mix 3 toleo lenye 5G.
Ukiwa kama mfuatiliaji mzuri wa bidhaa za Xiaomi utakumbuka vyema kuwa Mi Mix 3 sio mara ya kwanza kuletwa machoni pa watu lakini sasa tofauti ya toleo la sasa na lile lililopita ni kwenye teknolojia ya mawasiliano nikimaanisha kutoka kwenye 4G mpaka kuleta 5G.
Xiaomi ni moja ya kampuni ambayo imekuwa ikileta ushindani kwa wapinzani ambao wamezoeleka kushika nafasi za juu na kwa simu hii imeonekana kuendelea kuweka vile vitu ambavyo vipo kwenye Mi Mix 3 toleo lililopita:
>Muonekano+Kipuri mama
Kioo cha OLED kwenye simu hiyo kina urefu wa inchi 6.4 na kama toleo la nyuma pia mambo ni yaleyale kama ilivyo kwa toleo la 4G kuhusiana kutokuwa na uwazi kidogo katikakati (notch). Xiaomi wameamua kuanza kutumia kipuri Qualcomm Snapdragon 855 ambacho ndio cha karibuni kabisa pamoja na Qualcomm X50 modem wa ajili ya kuwezesha tewknolojia ya 5G kwenye simu husika.
>Kamera
Bidhaa hiyo ina kamera nne (4) kwa ujumla wake; kamera mbili za nnyuma zina MP 12 kila moja na kwa upande wa mbele kamera kuu ima MP 24 na nyingine imewekwa MP 2.

>Memori ya ndani+RAM
Raha ya simu iwe ns RAM kubwa ili kuwezesha kasi/ufanisi wa kifaa husika. Tukiangazia toleo jipya la Mi Mix 3 imewekwa GB 6/8 kwa 128GB, GB 8/10 za RAM kwa 256GB diski uhifadhi.
>Betri+Mengineyo
Uwezo wake wa betri sio mkubwa sana; ina 3200mAh, inatumia Android 9, rangi zake ni mbili tu-Bluu na Nyeusi, teknolojia ya kutumia alama ya kidole/uso ipo na kuanza kupatikana ni mpaka mwezi Mei.
Xiaomi Mi Mix 3 5G inategemewa kuuzwa kwa bei ya mwanzo kabisa $679|zaidi ya Tsh. 1,561,700. Vipi umeona upo umuhimu wa kuachana na toleo la 4G na kuhamia 5G?
Vyanzo: The Verge, TechCrunch, CNET