Maboresho ya programu endeshi ambayo Apple wanatoa kila mara ya muda fulani yanaonekana kupokelewa vizuri kwani asilimia themanini ya bidhaa za Apple zinatumia iOS toleo la 12.
Kwa wanaomiliki kifaa cha kidijiti kutoka Apple bila shaka walishawishika kuhama toleo la nyuma na kuhamia iOS 12 kutokana na sifa/maboresho ambayo yamewekwa kwenye toleo hilo.
Imekuwa ni kawaida kwa Apple kutoa takwimu za idadi ya vifaa kutoka kwao vikitumia mfumo endeshi wa karibuni kabisa na kwa mujibu wa taarifa iliyotoka Feb 24 kuhusiana na hilo mambo yapo hivi:
83% ya budhaa za Apple zilizotoka miaka minne iliyopita vinatumia mfumo endeshi-iOS 12. 80% ya vifaa vyote vya Apple vinatumia iOS 12 au juu ya hapo.
Mwanzoni mwaka huu (Januari Mosi 2019) 75% ya bidhaa za Apple zilikuwa zinatumia iOS na 78% ya bidhaa zilizotoka miaka minne nyuma zilikuwa zimeshahamia iOS 12.
Kwa takwimu hizo iOS 12 imepewa alama 4/5 ya ubora wa bidhaa zote kutoka Apple ambazo zinatumia toleo hilo. Vipi na wewe bado unatumia toleo la nyuma zaidi au umehamia kwenye toleo la karibuni zaidi?
Vyanzo: GSMArena, 9to5Mac