Betri (Battery) ni kitu muhimu sana kwenye simu ambapo watuamiaji wengi huwa makini sana simu zao zisiishe chaji (charge), lakini hii ni changaamoto kutokana na uwepo wa programu (Apps) zinazotumia zaidi betri ya simu na hizi Apps tunazitumia mara kwa mara katika shughuli zetu za kila siku.
Kuna programu (Apps) nyingi sana kwa simu za Android kwenye Google Play Store na simu za iPhone kwenye App Store ambazo zinatoa huduma zinazofanana, lakini watumiaji wengi hupakua programu (Apps) ambazo ni maarufu (Ambazo hutumiwa na watu wengi). lakini pia hizi Apps maarufu zinazotumiwa na watu wengi ndiyo humaliza au hutumia zaidi betri (battery) ya simu yako.
Zifuatazo ni programu (Apps) ambazo hutumia zaidi betri kwenye simujanja yako.
- Fitbit
- Uber
- Skype
- Airbnb
- Tinder
- Bumble
- Snapchat
- Zoom
- YouTube
- Booking.com
- Telegram
- Linkedln
Jambo moja ni kwamba hizi ni programu (Apps) ambazo hutumiwa zaidi au hutumiwa mara kwa mara na watu, na unaweza kuwa nazo zaidi ya moja kwenye simu yako lakini ukweli ukweli ni kwamba hizi programu (Apps) zinatumika pasipo kuifungua (run on background) hivyo hutumia sana betri (battery) ya simu yako, kama kuna programu (Apps) ipo kwenye orodha niliyotaja hapo juu na huitumii mara kwa mara unaweza kuindoa ili kupunguza matumizi ya betri.
Kutokana na utafiti uliofanywa na shirika la pCloud imeonyesha kuwa hizo ni programu (Apps) zinazotumia zaidi betri ya simu yako.
MITANDAO YA KIJAMII (SOCIAL MEDIA APPS)
Kati ya programu (Apps) 20 zinazotumia zaidi batri (battery) kwenye simu yako, kuna programu sita za mitandao ya kijamii nazo ni Facebook, Instagram, Snapchat, Youtube, WhatsApp na Linkedin, zaidi ya hapo hizo programu hutumia pia photos, wifi, locations, microphone kwenye simu pindi ambapo wewe huzitumii (run on background).
JINSI YA KUZUIA HIZI PROGRAMU KUTOTUMA ZAIDI BETRI YA SIMU YAKO.
Wengi huwalazimu kuziondoa baadhi ya programu hizo ili kupata nafasi na pia kupunguza matumizi ya betri, lakini pia unaweza kuamua kuzizuia zisifanye kazi pindi ambapo huzitumii (turn off background activity), kwenye upande wa simu za Android kuna programu nyingi zinafaya kazi pasipo kuziruhusu ila pindi unapozizuia kufanya hivyo hautopokea jumbe (notifications) mfano kama kuna ujumbe umeingia kwenye Instagram au mtandao wowote ambao umeuzuia hautoona mpaka ufungue hiyo programu (App) ndipo uweze kusoma hizo jumbe (notifications).
- Nenda kwenye simu yako ya Android kwenye upande wa settings
- Nenda sehemu imeandikwa “Battery”
- Chagua sehemu ya “Optimize battery use” iliyopo kwenye upande wa “Advanced settings” kwenye mipangilio (settings menu)
- Chagua programu (App) unayotaka kuizuia kisha bofya “Don’t optimize”
imekuwa ni kero kwa watumiaji wengi wa simujanja (smartphones) betri za simu zao kuisha mapema sana na hii husababishwa na matumizi ya simu yako ikiwepo na matumizi ya programu (Apps) ambazo humaliza betri kwa kiasi kikubwa, unashauriwa kuondoa baadhi ya programu ambazo huzitumii mara kwa mara au kuzizuia programu hizo kutofanya kazi pindi huzitumii inasaidia kupunguza matumizi ya betri (battery)
No Comment! Be the first one.