Microsoft inaleta toleo jipya la Windows 10 ambalo litaweza kuwa ruhusu watumiaji wa simu za windows 10 na Android kuweza kuona notification za simu zao kwenye kompyuta.
Microsoft wametangaza swala hili mwishoni mwa mkutano uliofanyika huko San fransisco mwishoni mwa wiki.
Huduma hii inayojulikana kama notification mirroring kwa kuanzia itafanya kazi ndani ya app ya cortana lakini baadae itakuwa inajitegemea ikifanya kazi katika OS hiyo mpya ya windows.
Bado haijajulikana kama ni lini update hii itatoka kwaajiri ya watumiaji wa kawaida lakini wengi wanategemea itapatikana katika sherehe ya kuazimisha mwaka mmoja wa Windows 10 ambayo ilizinduliwa mwaka jana mwezi Julai tarehe 29.
Microsoft wanaangalia namna ya kufanya hili liweze kufanya kazi pia katika simu za iPhone ambazo kwa sasa hazitapata huduma hii, utakapo iona notification katika kompyuta na kuipotezea basi hata katika simu itakuwa imepotezewa.
Kwa sisi watumiaji wa Android hii ni nafuu kwa maana kwamba sasa hautahitaji kuangalia simu yako wakati ukiwa ukiwa-busy unafanya kazi katika kompyuta yenye Windows 10.
Pamoja na hii huduma Windows 10 inategemewa kuja na mambo mengi baadhi ni pamoja na jinsi ambavyo start menu itaonekana.
Chanzo: Mtandao wa TechnoBuffalo