fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Android Maujanja

Njia Za Kupata Data Zako Zilizopotea (Zilizofutwa) Katika Kifaa Cha Android!

Njia Za Kupata Data Zako Zilizopotea (Zilizofutwa) Katika Kifaa Cha Android!

Spread the love

Sio kitu kipya wote tumeshawahi fanya, kwa bahati mbaya tulishawahi kufuta taarifa zetu kama vile picha au hata video. Kama ikitokea hivyo tena usikasirike, TeknoKona inakuletea njia.

Sawa kama nlivyosema kuwa unaweza ukapata taarifa zako zote ambazo ulifuta kwa bahati mbaya lakini kabla ya kuzipata kuna mambo inabidi uyafanye

• Usihifadhi (save) kitu kingine chochote katika simu kifaa chako au izime mpaka ukiwa unampango wa kufufua vitu vyako
• Zima WiFi na njia za mawasiliano za 2G/3G ili masashisho (update) yanayofanyikaga automatiki yasifanyike. Kumbuka kama yakifanyika, mafaili mapya yanaweza jiweka juu ya yale ambayo unataka kutafufua

Tuifahamu Njia

Kama Mafaili Yako Yapo Katika Memori Kadi

Ukishaona mafaili yako yamefutika bahati mbaya – au hata kwa makusudi – kitu kinachofuata ni kuunganisha kompyuta yako na simu kwa kutumia USB. Kuna baadhi ya matoleo ya vifaa vya android, ukichomeka USB katika kompyuta haijionyesha katika mfumo ule wa ‘kuonekana kama umechomeka Flash tuu’ .

SOMA PIA  Jinsi ya Kufungua na Kuandika Faili la PDF kwenye MS Word 2013

Kama simu yako haifanyi hivyo na una uhakika taarifa zako hizo zilikuwa katika sehemu ya memory kadi unaweza ukatumia adapta ya memori kadi hiyo na kuichomeka katika kompyuta ili isome mafaili yaliyomo ndani.

Sasa unaweza ukashusha programu ya Recuva katika kompyuta (Unaweza ukashusha ya bure au ya kulipia)

Bofya hapa Kushusha Recuva

Ukishafungua Recuva kitu cha kwanza ni kuchagua mafaili gani unayotaka kuyafufua katika kifaa chako (picha, video n.k). Unaweza ukachagua sehemu husika ambapo unataka mafaili ya eneo hilo yafufuliwe. Kitu cha muhimu cha kuweka akilini hapa ni kwamba program ya Recuva itaonyesha maeneo ambayo inaweza fufua mafaili yaliyofutika tuu.

Recuva Ikionyesha Mafaili Ambayo Unaweza Ukayafufua (Itakubidi kuweka Alama Ya Vyema Katika Mafaili Unayotaka Kuyafufua

Recuva Ikionyesha Mafaili Ambayo Unaweza Ukayafufua (Itakubidi kuweka Alama Ya Vyema Katika Mafaili Unayotaka Kuyafufua

Kingine cha muhimu ni kwamba unashauriwa kama ukimaliza fufua mafaili yako inabidi kwanza uyahifadhi (save) katika eneo lingine na kisha baadae ndio uyahamishie katika kifaa chako pale yalipofutika. Kujaribu kuyarudishia pale pale wakati unayafufua kunaweza kukaleta shida wakati mwingine. Kwa mfano kama ukiwa unafufua mafaili yako katika simu janja huna budi kuyahifadhi katika kompyuta yako na yakimaliza kuufufuka uyapeleke tena katika simu.

SOMA PIA  Jinsi ya Kufungua Spotify na Kusikiliza Muziki Mahali Popote

Kama Mafaili Yako Hayapo Kwenye Memori Kadi (Yapo Kwenye Simu)

Kama mafaili unayotaka kuyafufua yalikuwa katika simu na sio memori kadi basi unaweza kutumia njia hii. Kama hujarihusu njia chaguo la ‘Developer’ katika simu yako fanya hivyo kwa kwenda kwenye Settings > About Phone > Build Number au kwa simu zingine Settings > About Device > Build Number na kisha bofya katika eneo la namba hiyo (Build Number) mara 7. Ukishamaliza kufanya hivyo nenda katika Settings > Developer Options And USB Debugging. Mpaka hapo utakuwa na uwezo wa kutumia programu kama Recuva katika kufufua mafaili

Recuva Ikiwa Inafanya Kazi Yake

Recuva Ikiwa Inafanya Kazi Yake

Mpaka hapo nadahani umekuwa mtaalamu juu ya jambo la kufufua vitu eeeeh? (haha!). Fufua vitu vyako vya muhimu pindi tuu vinavyofutika kwa bahati mbaya.

SOMA PIA  Ongeza Kasi Ya Ushushaji (Download) Wa Vitu Kutoka uTorrent!

Kwa kutumia njia hii huweza ukawa na wasiwasi kuwa utakuja kupoteza vitu vyako na usivipate tena. Kama ukijitokeza hivyo unatumia Recuva tuu.

Niandikie sehemu ya comment hapo chini hii umeipokeaje? Je uko tayari kushiriki katika kufufua vitu, ningependa kusikia kutoka kwako. Tembelea teknokona kila siku kwa habari za kibabe zinazohusu teknolojia. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Comments

  1. […] Soma Pia – Njia za kupata Data zako zilizopotea (zilizofutwa) kwenye simu ya Android […]

  2. […] Soma Pia – Njia za kupata data zako zilizopotea/kufutwa ktk simu/tableti ya android […]

TeknoKona Teknolojia Tanzania