Kama tunavyojua kila baada ya muda wataalamu wa mtandao wa kijamii wa WhatsApp huleta masasisho (Updates) mbalimbali mapya kwa ajili ya kuboresha huduma zao.
Hivi karibuni imefahamika timu ya WhatsApp inajaribu kupima uwezo wa kuonesha status kwenye orodha za chats/mazungumzo ndani ya app hiyo.
Ripoti mbalimbali kutoka WABetaInfo zinaelezea kuwa wataalamu wa WhatsApp wanafanya majaribio ya kuonesha status moja kwa moja kwenye chats, status hizo zitaonekana kwenye picha ya mtumaji. Uwezo huu mpya utafanana na ule wa kwenye programu ya Instagram (Insta stories).


Wataalamu wa WhatsApp walitoa pia na picha mbalimbali kuonyesha muonekano mpya wa app hiyo mara baada ya uwezo huo mpya kuongezeka. Sasisho (Update) hili jipya la programu ya WhatsApp litaambatana na:
- Sasisho la kwenye kompyuta ambalo litakuja na uwezo mpya wa watu kupiga kura kwenye makundi yao.
- Emoji 8 za pekee zinazoweza kutumika kuonyesha maoni au hisia zako juu ya status uliyoangalia
WhatsApp bado haijatangaza rasmi ni lini itaachia rasmi masasisho haya lakini pia haijatangaza rasmi kuongezea vipengele hivyo katika masasiho yajayo kwa sasa ni majaribio tu yanayofanyika na si vinginevyo. Huenda katika hatua hii ya majaribio vipengele hivi vikapuuziwa na wakaongezea vingine au pengine utafiti zaidi ukahitajika na hivyo kuchelewesha kuachiliwa kwa vipengele hivyo.
Chanzo: Gadgets360
No Comment! Be the first one.