WhatsApp kupitia huduma yake ya channels imeongeza vipengele kadhaa ili kuhakikisha kuwa watu maarufu, chapa (brands) na vioo vya jamii kuweza kuwasiliana vizuri na mashabiki zao.
Kumbuka WhatsApp Channels ni njia nzuri sana ya kuwasiliana kwa pande zote mbili na mara nyingi mawasiliano hayo yamekaa kwa njia ya taarifa –njia moja—kutoka juu kwenda kwa mashabiki/wafuasi.
Vipengele Vilivoongezwa Ni;
Viboksi Vya Kupigia Kura (In-Stream Polls)
Kipengele hiki hakina tofauti kubwa sana na kile cha WhatsApp ya kawaida kabisa na hapa dhima yake kubwa ni katika kuhakikisha kuwa kuwa meseji hizi zinakua na changio kwa wadau wengi ndani ya chaneli husika.
Hii kwa mwenye chaneli ni kitu kizuri maana hapa anaweza hata akauliza swali kwa njia hii na akaweka majibu kwa njia ya machaguo.
Moja kwa moja chaguo ambalo litakua ni pendekezo kubwa kwa wafuasi litakua ndio sahihi, mfano msanii anaweza weka machaguo ya jina la album yake ijayo ili wafuasi wachague moja.
Jumbe Za Sauti (Voice Notes)
Hapa kama muhusika mkuu wa chaneli hiyo hataki kundika au anahisi kwa maandishi wafuasi wake wanaweza wasiipate mada yake vizuri anaweza akatuma ujumbe wa sauti.
Uzuri wa ujembe wa sauti unafanya upande kusudiwa ujione uko karibu zaidi na mtumaji wa ujumbe huo.
Hiki ni kitu kizuri kwa watu maarufu kufanya hivi mara kwa mara kwani hata mashabiki watajivunia kwa kiasi kikubwa kuwa katika chaneli hiyo.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je unaona ni kipengele gani kingine kiongezwe katika huduma hii ya WhatsApp Channels, niandikie hapo chini katika eneo la comment.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.