fbpx
apps, Intaneti, Kompyuta

Mambo 11 Yakushangaza Kuhusu Virusi vya Kompyuta

mambo-yakushangaza-kuhusu-virusi-vya-kompyuta
Sambaza

Virusi vya kompyuta ni swala ambalo limesikika mara nyingi; huku wengine wakiwa pia ni waathirika wa virusi hivi bila hata kuvifahamu vyema.

Kumekuwa na fikra na mitazamo kadha wa kadha kuhusu virusi hivi, mitazamo mingine ikiwa ya kweli na mingine ya uongo. Kwa mfano wengine huamini kuwa virusi hivi ni viumbe hai, wengine huamini vinaweza kumpata binadamu na wengine huamini kuwa ni kitu kisichoeleweka.

Ukweli ni kuwa virusi vya kompyuta ni programu kama programu nyingine lakini zlizotengenezwa kwa lengo la kuingilia au kuharibu utendaji kazi au mfumo wa kompyuta.

Naamini kwa kuwa unapenda maarifa, kuna mabo 11 ambayo ningependa nikushirikishe kuhusu virusi vya kompyuta.

1. Kuna jamii kuu tatu za virusi

Kwa sasa duniani kuna jamii kuu tatu za virusi ambazo ni “viruses (virusi), worms, and Trojan horses

”. Lakini vyote hivi vimetengenezwa kwa kufuata mfumo mmoja wa msingi kwa lengo la kutekeleza makusudi yanayokaribiana.

INAYOHUSIANA  WhatsApp: Watumiaji wa GB WhatsApp na WhatsApp Plus hatarini kufungiwa milele

2. Watengeneza virusi wengi ni wanaume

watengeneza virusi

Inaelezwa kuwa watengeneza virusi au programu hatarishi za kompyuta ni wanaume kati ya umri wa miaka 14 hadi 25. Inaelezwa kuwa ni wanawake wachache sana ndiyo waliobainika kujihusisha na utengenezaji wa virusi.

3. Watengeneza virusi wengi wameajiriwa

Uchunguzi unaeleza kuwa silimia 70 ya watengeneza virusi wengi, wameajiriwa na makampuni makubwa ya kihalifu kufanya hivyo.

4.Kirusi cha Melissa

ms

Kirusi cha Melissa kilichoibuka mnamo mwaka 1999, kilikuwa tishio hadi kusababisha Microsoft na makampuni mengine kuzima huduma zake za barua pepe hadi pale kilipoondolewa.

5. Kabla ya kukua kwa mtandao, virusi vilisambaa kupitia vifaa vya kuhifadhia data

disc

Inaelezwa kuwa kabla ya kukua kwa mtandao wa intaneti, virusi vya kompyuta vilisambaa kwa njia ya vifaa ya kuhifadhia na kuhamishia data hasa floppy disks. Wakati huo watu wengi walikuwa wakishirikishana mafaili na taarifa mbalimbali kwa kutumia vifaa hivi.

INAYOHUSIANA  Bill Gates asema anatumia simu ya Android, Ni samsung Galaxy S8?

6. Amazon ni mlengwa namba moja

Tovuti ya kuuza na kununua vitu kwenye mtandao ya Amazon.com, ndiyo mlengwa mkubwa wa uvamizi wa virusi ikifuatiwa na Apple pamoja na eBay.

7. Marekani iko hatarini zaidi katika uvamizi wa virusi

Takwimu zinaeleza kuwa kimataifa, Marekani ndiyo nchi iliyoko hatarini zaidi katika uvamizi wa virusi ikifuatiwa na Urusi.

8. Kutengeneza kirusi huko Marekani siyo kinyume cha sheria

Kuandika au kubuni kirusi nchini Marekani siyo kinyume cha sheria hadi pale utakapokitumia kufanya uhalifu. Hali hii ni tofauti na nchi nyingine kama vile Ujerumani na Finland ambazo zimeanza kuweka sheria juu ya udhibiti wa utengenezaji wa virusi vya kompyuta.

9. Virusi 6,000 huzalishwa kila mwezi

vr

Takwimu mbalimbali zinabainisha kuwa hivi leo takriban virusi vya kompyuta vipatavyo 6,000 huzalishwa kila mwezi.

10. Kirusi cha ILOVEYOU ndicho kibaya zaidi kuwahi kutokea

Kirusi cha kompyuta kinachofahamika kwa jina la ILOVEYOU ndicho kirusi kibaya zaidi cha kumpyuta kuwahi kutokea.

INAYOHUSIANA  Adobe Waja Na Adobe Scan, App Ya Ku'Scan Kwa iOs Na Android!

Kirusi hiki husambaa kwa njia ya barua pepe na huathiri mfumo mzima wa kompyuta. Inakadiriwa kuwa kimesababisha hasara ya dola bilioni 10 hadi 15 za Kimarekani.

11. Ukidukua Facebook utalipwa dola 500

fb

Nini? Dola 500? Ndiyo wahi fursa hii sasa. Ili kubaini udhaifu katika mfumo wa Facebook, kampuni hii hutoa dola 500 za Kimarekani kwa mtu yeyote atakayeweza kudukua au kuingiza virusi kwenye mfumo wa Facebook.

Neno la Mwisho

Ni wazi kuwa yapo mambo mengi kuhusu virusi vya kompyuta, lakini kwa haya machache naamini umepata maarifa. Ni vyema kufahamu kuwa virusi vya kompyuta vipo na ni hatari sana. Chukua tahadhari ya kulinda vifaa vyako kwa kutumia kinga-virusi (antivirus) bora leo.

Naamini umejifunza mengi; ikiwa una swali au maoni basi karibu utuandikie hapo chini. Usisahau kuwashirikisha wengine makala hii kutoka Teknokona.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Kornel Maanga

Kornel ni mfuasi mkubwa wa maswala ya kompyuta na msanifu mtandao toka mwaka 2008. Ana uzoefu mzuri katika maswala mbalimbali yanayohusu kompyuta na teknolojia. Amekuwa akifanya kazi mbalimbali kama vile kutengeneza tovuti, kutengeneza programu mbalimbali, usanifu picha na video bila kusahau uandishi wa makala kadha wa kadha katika tovuti na blog mbalimbali.