Apple Music ni moja katika ya masoko ya muziki yanalipa vizuri wasanii na watengenezaji wengine wa maudhui ya sauti.
Lakini kwa sasa Apple music nayo ina masharti mapya kwa waandaji wa maudhui hao, na kwa haraka haraka ni maamuzi mazuri.
Kwa haraka haraka ni kwamba kampuni ya Apple inauza bidhaa ambazo sio za kwake ni za wasanii (waandaji wa maudhui) lakini ili maudhui hayo yauzike ni lazima yawe yana ubora (quality) ya juu.
Kulingana na sababu hiyo imeamua kuwafanya waandaji hao wa maudhui kuchangamkia furusa ambayo wamewapa…
…yaani hapa wana mpango wa kulipa zaidi katika maudhui ambayo yameandaliwa katika ubora wa hali ya juu.
Kwa mfano kama ni msanii akiweka nyimbo ambayo ina ubora wa hali ya juu kuanzia katika uandaaji wake wa mdundo mpaka uimbaji basi msanii huyu atalipwa vizuri ukilinganisha na yule ambae hajafanya hivyo.
Kulingana na kwamba teknolojia yetu inazidi kukua kwa kasi, tunaamini hata wasanii ambao wanatengeza maudhui mazuri inabidi wapate zawadi juu ya jambo hilo” — walisema Apple.
Ni wazi kwamba katika majukwaa mengi ya maudhui kwa sasa wanataka kurusha maudhui yenye ubora wa hali ya juu ambayo hata watumiaji wake watapa kile kilicho bora zaidi.
Majukwaa ya muziki ndio kabisa kwa sasa yanuza ubora zaidi kuliko hata maudhui yenyewe maana wa teknolojia ya juu zaidi katika hili.
Niandikie hapo chini katika eneo la comment je wewe unakubaliana na jambo hili kwamba mwenye maudhui yenye ubora zaidi alipwe kikubwa kuliko yule mwenye maudhui yasiyo na ubora kwenye uaandaaji?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.