fbpx

Watumishi wa serikali kutumia TTCL sasa ni lazima!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Umaarufu wa shirika la mawasiliano nchini Tanzania, TTCL umeongezeka mara dufu katika miaka miaka ya karibuni ukilinnganisha na muongo mmoja uliopita. Idadi ya watumiaji wa kadi za simu-TTCL inatazamiwa kuongezaeka baada ya kuwa ni LAZIMA kwa watumishi wa serikali kutumia mtandao huo wa simu.

TTCL ambayo inaonekana kuimarika mwaka hadi mwaka kwa kuweza kurudi kwenye ushindani wa kibiashara na makampuni mengine ya simu kuifanya kuweza kufikisha wateja zaidi ya laki nne, mawakala kumi na moja elfu kwa idadi kulingana na taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Bw. Waziri Kindamba wakati wa kukabidhi hundi ya gawio kwa serikali kwa mwaka huu.

INAYOHUSIANA  Kifo Cha Mtandao Wa Vine Ndio Hiki! #Apps

Tukio hilo la kukabidhi hundi ya Tsh. bilioni 2.1 bilioni iliyopokelewa na rais Magufuli halikupita hivi hivi baada ya mkuu huyo wa nchi kutuoa mwezi mmoja kwa wizara, taasisi za serikali na watumishi wa serikali kuanza kutumia laini za TTCL mara moja kwa ukweli kwamba ni lazima tupende vya kwetu kwanza.

Watumishi wa serikali

Mei 21 2019: Tukio la kukabidhi kwa serikali hundi ya Tsh. 2.1 lililoshuhudiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Kindamba, rais Magufuli, Waziri wa Ujenzi, Mawasilaino na Uchukuzi, Mhandisi Isack Kamwelwe na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi-TTCL, Bw. Omary Nundu.

Rais Magufuli ameona upo ulazima wa kulazimisha watumishi wa serikali na hata chama anachokiongoza kuanza kutumia mtandao huo wa simu kwani bila kufanya hivyo ile dhana ya kupenda vya kwetu kwanza itakuwa ni ya maneno tuu na hatimae kuendelea kuneemesha makampuni mengine ya simu na badala ya kupenda kitu cha kwetu kwanza.

INAYOHUSIANA  Google wanajiandaa kuja na toleo jingine la Android; Ila kuna ulazima kweli?

Kuhusu TTCL kukodi minara

Ingawa TTCL imefanikiwa kutoa gawio kwa mara ya pili mfululizo ambalo limekwenda moja kwa moja serikalini (Wizara ya Fedha na Mipango) rais Magufuli ameshangazawa na shiirka hilo kutokuwa na minara yake tenyewe hivyo basi kuingia gharama ya kukodi miundombinu hiyo kutoka kwa makampuni mengine kitu ambacho kinaigharimu kampuni hiyo Tsh. milioni 700-800 kwa mwezi.

Dkt. Magufuli amesema ipo haja ya kuiwezesha kampuni hiyo ili iweze kujenga minara yake yenyewe na kuacha kabisa masuala ya kukodi na hivyo kuwezesha huduma za mawasiliano kwa wateja wake.

Vipi wewe msomaji wetu huduma za TTCL zimekuvutia kiasi cha kwamba una kadi ya simu kutoka shirika hilo ukiitumia kwa mawasiliano? Tupe maoni yako na hiyo ndio Tanzania inayojitahidi kufanya wananchi wake wapende vya kwao kwanza.

Chanzo: Gazeti la Mwanachi

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.