Ingawa kasi ya intaneti na uwezo wa vifaa mbalimbali kuhimili huduma ya intaneti ya kasi kubwa unazidi kukua bado watu wanaona tovuti (websites) hazifunguki kwa kasi zaidi.
Kasi iliyopo badi hairidhishi. Na ni kutokana na hili basi kundi la watafiti wa MIT(Massachusetts Institute of Technology) kitengo kinachojihusisha na sayansi ya kompyuta pamoja na akili-feki za kiteknolojia wamefanikiwa kupata njia ya kuongeza kasi ya mtandao kufunguka bila kuongeza kasi ya huduma ya intaneti inayotumika.
Maboresho haya yametambulishwa na kundi la wasomi la chuo cha MIT (Massachusetts Institute of Technology – kitengo cha Computer Science and Artificial Intelligence Laboratory (CSAIL))
Wametengeneza mfumo walioupa jina la Polaris ambao utaweza kutambua haraka mahitaji ya tovuti inayofunguliwa ili kuhakikisha kila kitu kinaenda sehemu yake kama inavyotakiwa kwa wakati ili kufanya tovuti husika ikamilike kwa haraka zaidi.
Jinsi vivinjari (browser) kama vile Chrome na Firefox vinavyofanya kazi ni kwa kujifunza code zinazotumika kwenye tovuti husika pale zinapoanza kuzingua, ila wakati mwingine huwa vivinjari hivi vinakutana na vitu vipya na hivyo kujikuta vinaitaji mahitaji mengine ili kufanikiwa kufungua tovuti husika katika hali nzuri, utaratibu huu huwa unaongeza muda wa tovuti husika kufunguka.
Shughuli ya vivinjari kutafuta kujua zaidi kuhusu code zilizotumika katika tovuti inazozifungua huongeza sekunde kadhaa katika muda unaochukua kufungua tovuti husika.
Mfano walioutumia kuelezea;
- Unaposafiri kwenda mji flani, saa nyingine ndio unatambua ya kwamba kuna miji mingine ya jirani ambayo ni mizuri pia na hivyo unaamua kwenda kabla ya kurudi kwako…ukifika kwenye mji mwingine napo unajifunza kuhusu mji mwingine.
- Ila kama mtu angekupatia orodha ya miji hiyo mapema kabla ya wewe kuanza safari hiyo basi angekusaidia wewe kujipanga vizuri na hivyo kuokoa muda wa safari husika.
- Basi hapo ndipo ugunduzi wao unaposaidia vivinjari, kuweza kufahamu mahitaji ya tovuti zinazofunguliwa mapema zaidi na hivyo kuweza kuzifungua kwa haraka zaidi.