fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Afya Teknolojia

Project BLAID – Toyota waja na Kifaa kusaidia Wasioona Kutembea bila Msaada

Project BLAID – Toyota waja na Kifaa kusaidia Wasioona Kutembea bila Msaada

Spread the love

Kampuni nguri katika utengenezaji wa magari ya Toyota wametambulisha rasmi kifaa ambacho wamekuwa wakikifanyia kazi kwa muda sasa kwa ajili ya kuwasaidia watu wasioona (vipofu) katika kuweza kutembea bila msaada.

Kwa miaka mingi watu wenye matatizo ya kuona wanaitaji vitu kama fimbo, mbwa n.k katika kuwasaidia kutembea. Toyota wametambulisha rasmi mradi walioupa jina la ‘Project BLAID’ ambapo wanategemea kuweza kuanza kufanyia majiribio kifaa hicho hivi karibuni.

Kifaa hicho ambacho kitavaliwa na mtu eneo la mabega kitaweza kumuelekeza mtu na kumtaarifu kuhusu vitu vilivyokatika eneo lake. Mfano kama ni gari, ukuta n.k.

Toyota Project BLAID

Kifaa hicho kikiwa kimevaliwa mabegani.

Inategemewa mvaaji atapata taarifa zitakazoweza kumsaidia kutembea ndani maeneo kama vile maofisini na ata kwenye maduka makubwa (malls) huku kifaa hicho kikiweza kumpa taarifa juu ya vitu kama vile – choo, ngazi, milango n.k.

Kifaa hicho ndani yake kinakuja na kamera kadhaa kwa ajili ya kuweza kusoma mazingira, pamoja na spika kwa ajili ya kumpatia mvaaji taarifa kuhusu mazingira yake.

Toyota wanasema wanazidi kuifanyia teknolojia hiyo maboresho ili kuweza kuongezea kifaa hicho uwezo wa kutambua sura na vitu vingine mbalimbali (facial recognition & object identification).

SOMA PIA  Zuia watu kukusambazia vitu vyao kupitia Google Drive

Tayari Toyota wamepata sifa sana kutokana na juhudi zao katika project hii. Wenyewe wanadai ni jambo ambalo wameamua kulifanya kama juhudi zao katika kuleta maana zaidi ya msemo wao wa kibiashara wa “Lets Go Places” – yaani ‘Twendeni Sehemu/Pahali’ hili likimaanisha kupitia utumiaji wa magari yao ya Toyota.

SOMA PIA  Motorola RAZR ipo njiani kuja lakini kivingine

Video kutoka Toyota kuhusu Project BLAID;

Kifaa cha “BLAID” Kitaanza kupatikana lini?

Kwa sasa bado wanafanya maboresho, na muda mrefu wataanza kufanya majaribio ya awali (beta testing)..hivyo bado ni mapema kusema ni lini kifaa hicho kitaingia sokoni na kuna uwezekano ata jina likabadilika.

Je una maoni gani juu ya teknolojia hii kutoka Toyota? Tuambie kwenye comment

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania