fbpx

Snapchat yajiandikisha katika soko la hisa! #Apps

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Mtandao wa Snapchat siku ya Alhamisi uliingia katika vichwa vya habari vya mitandao mingi ya biashara baada ya kuanza mchakato wa kujiunga na soko la hisa, Snapchat  imejiandikisha kama SNAP katika soko la hisa la New York maarufu kama NYSE.

hisa

Snap ambayo ndiyo kampuni ya mama ya mtandao wa snapchat imeanza mchakato wa kuuza hisa zake na inategemewa kampuni hii itaweza kukusanya hadi dola za kimarekani bilioni 25, kama matarajio haya yatafikiwa basi kampuni hii itakuwa imevunja rekodi ya makampuni mengine na pengine itakuwa na thamani katika soko hatakuishinda Twitter.

INAYOHUSIANA  Kuna uwezekano Google kutengeneza simu yake mwaka huu! #Ripoti

Katika taarifa yake iliyowasilishwa katika undikishaji huo Snapchat imesema kwamba hadi mwaka jana mwishoni ilikuwa na watumiaji hai milioni 158 kila siku, pia taarifa hiyo ilisema kwamba kuna takribani snap bilioni 2.5 ambazo zinatengenezwa kila siku.

Baada ya kuanzisha mchakato wa kujiandikisha katika soko la hisa kampuni hii intakiwa kuwashawishi wawekezaji ili waweze kuwekeza pesa katika hisa za kampuni hii, jambo hili sio rahisi hasa ukizingatia ukweli kwamba aina ya biashara Snapchat inafanya sio kitu watu walikizoea.

INAYOHUSIANA  Fungua Faili La PDF Bila PDF Reader Katika Kompyuta!

Wengi walisema snapchat haitadumu, wengi walitabiri kwamba ingekufa kama ambavyo mitandao mingi inayoanzishwa hufa lakini hali haikuwa hivyo hii ni fundisho kwa wajasiriamali wadogo kutovunjika moyo pindi wachambuzi wanapo ponda mawazo yao.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus.

Habari hii imeandikwa kwa msaada wa vyanzo mbalimbali mtandaoni.

 

Facebook Comments

Sambaza
Share.