Jambo la kuweka neno siri/nywila imekuwa ni kitu ambacho kimezoeleka na pengine mtumiaji hatojihisi yuko salama kama hatoweka nywila kwenye simu yake.
Udukuzi unaweza ukafanyika hata bila ya wewe kutarajia kama mtu angeweza kufahamu password yako ila tambua ya kwamba jinsi unavyoshika simu janja yako kunaweza kumfanya mtu mwingine akajua neno siri unalotumia kwenye simu yako kwa urahisi.
Katika utafiti uliofanyika katika chuo kikuu cha Newcastle ulibaini kuwa asilimia 70 ya nambari zote za siri zenye tarakimu nne zilifahamika baada ya kujaribu mara moja tu na kwa asilimia 100 baada ya kujaribu mara tano.

Simu nyingi aina ya simu janja na tabiti zimewekwa sensa ingawa kuna tovuti nyingi na programu za simu haziombi ruhusa kabla ya kutumia programu hizi jambo linalopelekea kuwa rahisi sana kwa programu mbaya kupata taarifa kutoka kwenye simu husika.
Wataalamu wamegundua kwamba kila unachofanya katika simu iwe ni kupiga simu, kuandika ujumbe mfupi wa maneno au kutafuta kitu hupelekea mtu kuishika simu kwa njia fulani ya kipekee.
One Comment
Comments are closed.