fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

tecno

Infinix simu Uchambuzi

Uchambuzi wa Infinix Smart 4, Uwezo na Sifa yake

tecno

Kampuni ya Infinix inafahamika kwa matoleo ya bei ya chini yenye kiwango kizuri cha ubora, na simu yao ya Infinix Smart 4 inadhihirisha hilo. Ni simu nzuri, hasa kwa bei ya chini yenye mfumo endeshi wa Android, betri nzuri na camera nzuri pia.

simu ya infinix smart 4

Muonekano wa simu ya Infinix Smart 4

 

Simu hii iliingia sokoni rasmi tarehe Oktoba 2019.

SOMA PIA  Utafiti: iPhone ni za wanawake masikini, Huawei ni kwa wanaume wenye nazo!

Sifa za simu hii ni kama;

  • Kioo (Display) cha teknolojia ya LCD chenye ukubwa wa inchi 6.6
  • Prosesa ya Mediatek MT6761 Helio A22
  • Mfumo endeshi wa Android 9.0 uliorahisishwa (Go Edition).
  • RAM ya GB 1 na diski uhifadhi ya GB 16, na pia kuna toleo la GB 64
  • Kamera ya nyuma yenye megapixel 8 kwa toleo la GB 16, megapixel 13 kwa toleo la GB 64 na kamera ya mbele/selfi yenye megapixel 5.
  • Betri yenye uwezo wa 4000 mAh
SOMA PIA  Mmoja wa waanzilishi wa Android kuja na simu ya kushindana na iPhone

Simu hii inasapoti teknolojia ya mawasiliano ya 4G, pia Bluetooth na WiFi. Ina teknolojia ya usalama ya alama za vidole (fingerprint). Inakuja na uwezo wa kusikilia redio katika mfumo wa FM.

tecno

smart 4 inifinix

Ina sehemu ya kuchomeka earphones na sehemu ya kuchomeka waya wa chaji aina ya microUSB 2.0 . Ina matoleo matatu ya rangi, Nyeusi (Midnight Black), Samawati (Quetzal Cyan) na Zambarau (Cosmic Purple).

SOMA PIA  Google watambulisha simu mpya, zifahamu Google Pixel na Pixel XL

Bei: Kwa wastani wa Tsh 200,000 kwa toleo la GB 16, na 230,000 – 240,000 kwa toleo la GB 64.

Je una mtazamo gani juu ya toleo hili la Infinix Smart 4?

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania