Simu ya Nokia C1 kutoka kampuni ya Nokia ni simu yenye muonekano mzuri na yenye kufaa kwa bei ya chini kabisa. Simu hii inakuja na mfumo endeshi wa Android uliorahisishwa (Android Go)
Simu hii ilitolewa rasmi Disemba 2019.
Android Go ni toleo spesheli kutoka Google linalohusisha Android ambayo sio nzito sana na hivyo inafaa sana kwa simu za kiwango cha chini hadi kati.
Nokia C1 ni simu ya bei nafuu yenye muonakano na uwezo mzuri wa kushindana na ata simu za bei ya juu zaidi yake.
Sifa na Uwezo wa Nokia C1:
- Kioo (Display) cha teknolojia ya LCD chenye ukubwa wa inch 5.45.
- Mfumo endeshi (OS) wa Android 9.0 Go Edition.
- RAM ya GB 1 na diski hifadhi ya GB 16, na inakubali memori kadi – MicroSD
- Kamera ya nyuma yenye megapixel 5 na kamera ya mbele yenye megapixel 5. Ina taa ya flash mbele na nyuma.
- Betri yenye uwezo wa 2,500mAh.
- Inakuja na teknolojia ya FM Redio
Simu hii haisapoti teknolojia ya mawasiliano ya 4G lakini inazo teknolojia za Bluetooth na WiFI. Pia, ina sehemu ya kuchomeka earphones na sehemu ya kuchomeka waya wa chaji aina ya microUSB 2.0. simu hii hupatikana katika rangi mbili, Nyeusi (Black) na Nyekundu (Blue).
Kumbuka simu za Nokia zinatengenezwa na kampuni ya HMD kwa leseni kutoka Nokia.
No Comment! Be the first one.