Kwa mara ya kwanza Twitter imewaonya (kwa barua pepe)baadhi ya watumiaji juu ya uwezekano wa watu wanaodhaminiwa na serikali ku-hack (kudukua) akaunti zao.
Onyo hili limeenda moja kwa moja kwa watumiaji ambao Twitter wanamini kwamba akaunti zao zinaweza zikawa zimeshambuliwa na udukuzi huo.
Hii ni mara ya kwanza kwa mtandao wa twitter kutoa onyo juu ya udukuzi unaodhaminiwa na serikali, mitandao kama Facebook na Google yenyewe imekwisha wahi kufanya kitu kama hiki siku za nyuma.
Ingawa Twitter wamekubali kwamba kweli kwamba walituma barua pepe kwa baadhi ya watumiaji lakini wamekataa kutoa taarifa zaidi juu ya swala hilo,lakini kwakuwa vibandiko (tweets) huwa wazi kwa mtu yeyote basi bila shaka wadukuzi hawa watakuwa walikuwa wanatafuta taarifa kama anuani za barua pepe, IP address ama namba za simu.
Wadukuzi wanaodhaminiwa na serikali
Kwa kimombo State sponsored hackers hawa ni wadukuzi ama wanaofanya udukuzi na kulipwa na serikali au wanafanya udukuzi kuisaidia serikali kwa sababu wanaunga mkono sera za serikali husika. Mfano wa wadukuzi wanaodhaminiwa na serikali ni Syrian Electronic Army ambao wao wanafanya udukuzi kwa ajiri ya kuisadia serikali ya Syria kushinda vita yake dhidi ya waasi, SEA kwa mfano hushambulia mitandao mbali mbali kama ya magazeti na vyombo vingine vya habari na kuweka habari zinazo muunga mkono Assad.
Nani walipata barua pepe hizo kutoka Twitter!?
Hajijulikani ni kundi gani la watumiaji wa twitter hasa waliopewa onyo ilo ila watu wachache walio jitokeza na kukili kwamba wamepewa onyo na Twitter ni pamoja na waandishi wa habari, wanausalama, wanasayansi pamoja na wachunguzi.
Ieleweke kwamba ingawa hii sio mara ya kwanza kwa Twitter kutoa taarifa kwa watumiji wake juu ya uhalifu wa kimitandao, mwaka 2013 Twitter iliwajulisha baadhi ya watumiaji wake juu ya uwezekano wa wizi wa passwords na anuani za barua pepe.
Hatua hii ya Twitter inawapa moyo watumiaji wengi wa mtandao huo kwamba hatakama watashambuliwa na serikali watajulishwa. Kwa hapa kwetu Tanzania bado hatujasikia kama kuna mtu alipata barua pepe hiyo ikimuonya juu ya shambulio la udukuzi! kama uliipata barua pepe hiyo ama unamjua mtu aliyepata onyo hilo tunaomba utujulishe katika Facebook Twitter ama Instagram
No Comment! Be the first one.