fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
simu Uchambuzi

Hii ni Simu janja Yenye Uwezo wa Kukaa na Chaji kwa Zaidi ya Siku 10

Hii ni Simu janja Yenye Uwezo wa Kukaa na Chaji kwa Zaidi ya Siku 10

Spread the love

Simu janja yenye uwezo wa kukaa na chaji kwa zaidi ya siku 10? Haraka haraka jambo hili linaonekana bado ni ndoto ila tayari kuna kampuni ambayo imedai imefanikisha jambo hili na simu zake zitaanza kupatikana mapema mwezi wa kwanza, 2016.

Simu janja hiyo inakuja na betri lenye kiwango kikubwa cha uhifadhi chaji wa mAh 10,000 italetwa na kampuni iitwayo Oukitel. Wenyewe wanasema kwa matumizi ya ‘kawaida’ wanategemea simu hiyo iweze kukaa na chaji kwa zaidi ya siku 10, wanasema kutegemea na utumiaji inaweza fikisha hadi siku 15.

Oukitel K10000

Oukitel K10000

Kampuni hiyo tayari miezi kadhaa nyuma ilishawahi kutoa simu janja yenye kiwango kikubwa cha uhifadhi chaji wa mAh 6000.

SOMA PIA  Kampuni ya teknolojia ya kifedha kutoka Kenya Zanifu imepata $1M ili kuziba pengo la kifedha wakitazamia kupanua huduma zao Ghana na Uganda.

Simu hii ya kiwango cha chaji cha mAh 10,000 itachukua jina la Oukitel K10000 na inakuja ikitumia toleo la Android 5,1 Lollipop.

Kupitia simu hiyo utaweza pia kuitumia kama vile ‘powerbank’ ili kuweza kuchaji simu yako nyingine ya ziada. 🙂

Sifa zinginezo za Oukitel K10000

  • Kioo (display) ya Inchi 5.5 HD (720X1280)
  • Prosesa – 1GHz quad-core MediaTek MT6735
  • RAM GB 2
  • Diski Uhifadhi (Storage) – GB 16 na uwezo wa kutumia kadi ya microSD
  • Kamera ya mbele ya MegaPixel 8 na ya selfi MegaPixel 2
SOMA PIA  Pixelbook: Kompyuta ya kwanza kutoka Google yenye 'Kisaidizi binafsi'

Kamera ya mbele inakuja na teknolojia za HDR, kutambua sura (face detection), uwezo wa kupiga picha za panorama n.k

Kimawasiliano inakuja na teknolojia za GPRS/EDGE na 3G, pia Bluetooth na WiFi.

Kwa sasa simu hiyo ishaanza kuuzwa kupitia mtandao wa GearBest kwa takribani dola 240 za Marekani, wanaolipia kwa sasa wataanza kuipata simu hiyo mwezi wa kwanza ambapo ndio pia itaanza kupatikana katika nchi zingine.

SOMA PIA  Mchina aliyewalaghai Apple kuchukua iPhone ghushi kama vifaa halisi vyenye thamani ya Dola Milioni 1 Ametiwa hatiani na kuhukumiwa

Vyanzo: Edgadget, NDTV na GearBest

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania