fbpx

Jinsi ya Kuondoa Lock Pattern ama Password Uliyoisahau katika Android

4

Sambaza

Makala hii itakusaidia kuweza kuondoa pattern ama password (nywila) uliyosahau katika simu yako (Android), zipo njia nyingi kutegemea na aina ya simu au toleo la Android ambalo simu yako inatumia.

Kwa kutumia barua pepe yako na password ya akaunti ya Google.

Simu zote ambazo zinatumia Android Kitkat ambayo ni toleo la 4.4 na nyingine zote ambazo ni matoleo ya nyuma ya hili zenyewe ni rahisi pindi unaposahau password yako, katika kundi hili la simu pindi tu unaposahau pattern ama password yako simu yako itakutaka uingize barua pepe na password yako ya Google ambayo ulijiandikishia katika simu hiyo na kisha simu yako itafunguliwa.

Angalizo! njia hiyo itafanya kazi iwapo umewasha data katika simu.

INAYOHUSIANA  Vipya kutoka BlackBerry na Alcatel kuja karibuni

Kwa kutumia Android Device Manager.

Njia hii simu zote ambazo katika zimewezeshwa programu hii, vile vile njia hii itafanikiwa iwapo tu wakati huo intaneti ya simu itakuwa imewashwa. njia hii inaweza sio tu kubadilisha password ya simu kwenda katika password yako mpya ila pia inaweza kusaidia kufuta mafaili yote yaliyo ndani ya simu – hii ni muhimu kama simu imepotea au kuibiwa.

Fuata hatua zifuatazo kufungua simu uliyoifunga.

  1. Tembelea google.com/android/devicemanager kupitia katika simu nyingine ama kompyuta
  2. Ingia kwa kutumia barua pepe pamoja na password yako uliyotumia kusajilia katika simu iliyojifunga
  3. Tafuta na chagua kifaa ambacho unataka kukifungua (maana kama una vifaa zaidi ya kimoja  ulivyo visajili katika huduma hii vyote vitaonekana hapa)
  4. Chagua Lock na uinigize password ya muda kisha bonyeza Lock tena
  5. Baada ya hapo unatakiwa uone meseji ikithibitisha kuwa kufaa chako kimebadilishwa password
  6. Wakati huu katika simu utaona sehemu ya kuandika password inatokea hapa jaza ile password yako mpya.
  7. Ingiza pasword na uende moja kwa moja kuiondoa pasword hiyo ya simu yako.
INAYOHUSIANA  Oreo yafika kwenye Samsung Galaxy J7 Prime

Kufungua simu kwa Apps mbali mbali.

Watengenezaji mbali mbali wa simu wanakuwa na application zao binafsi kwaajiri ya kusaidia kufungua simu iliyojifunga na password kusahaulika, siku zijazo tutaiongelea kwa marefu njia hii kwa undani. Kwa ufupi ni kwamba njia hii inafanya kazi kama njia iliyopita tofauti ni chache na zinatokana na ukweli kwamba zinatengenezwa na watu tofauti.

android_lockscreen

Screen ikiwa imefungwa kwa pattern

Kufungua simu kwa kurudisha industrial default settings 

Njia hii hufuta kila kitu katika simu na kuifanya iwe na mpangilio ule ule iliokuwanao wakati inatoka kiwandani. Njia hii ni ndiyo kimbilio la mwisho kwa ikiwa kama mtu umesahau pattern na password, njia hii hufuta mipangilio  yoote ya simu na hifanya simu iwe kama mpya na kufuta passwords ama patterns zilizo katika simu.

INAYOHUSIANA  Nokia kuingiza dola 3.48 kwa kila simu yenye 5G

Makala zinazofuata nitaandika kipengele kimoja kimoja kwa kirefu zaidi. Tuambie je wewe ulitumia njia ipi kuondoa pattern ama password kwenye simu yako? Endelea kutembelea TeknoKona.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

4 Comments

  1. Tuna appreciate kazi ako bro. Ila naushauri kidogo apa…ni vema ukiwa unaambatanisha video or more photos hasa pale unapotoa maelekezo ili kuweza kuturahisishia kukuelewa zaidi….NICE WORK BRO KEEP UP!!!!!

Leave A Reply