fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps Mtandao wa Kijamii Teknolojia

Tuangalie Maboresho Katika App Ya SnapChat!

Tuangalie Maboresho Katika App Ya SnapChat!

Spread the love

Licha ya App hii kukua kwa kasi ndani ya kipindi cha mda mchache bado haijatosheka na ukuaji huo. App ya snapchat bado inaendelea kufanya maboresho na vipengele kadha wa kadha. Kumbuka hapo awali App hiyo (SnapChat) iliongeza ‘Filter’ mbali mbali kama lenzi na zingine.

Yote haya yanafanyika kwa lengo la kuwavutia watumiaji wapya katika App hii na hata wale watangazaji. Ili kufanya hivyo Snapchat imeingiza vipengele vingine katika App Yake. Vipengele hivyo ikiwa ni kama hatua ya App kukua kimaboresho zaidi.

snapchat-lenses

Lenzi Za Picha Katika SnapChat

Maboresho au vipengele vipya vilivyoongezwa ni vya aina tatu katika video yaani; fast-forward, slow Motion na rewind ikiwa na maana ya Kusogeza mbele kwa kasi, Kupunguza kasi na Kurudisha nyuma. Vipengele hivi vitatu vitaonekana katika Snap za video tuu na sio zile za picha

snapchat-video-filters

‘Filter’ Za Video Katika App Ya SnapChat

Fast Forward: Hii inafanya video kucheza katika spidi ya kasi sana na ni nzuri kwa wale wanotengeneza video zenye ‘effects’ au hata comic

Slow Motion: Hii inapunguza kasi ya video na kumfanya mtazamaji aone vitu vingi ambavyo pengine asingeviona kama ingekuwa inacheza kawaida.

Rewind: Hii inakuwezesha kuangalia video kwenye kasi ile ile ila kwa kinyume yaani kutoka mbele kurudi nyuma

Mfano Wa Filter Ya Rewind Katika Video Ya SnapChat

Mfano Wa Filter Ya Rewind Katika Video Ya SnapChat

Ukiachana na vipengele hivyo vipya vitatu  katika video pia snapchat imeleta maboresho na haya yamejikita kwa watumiaji wa iOs kutokana na kuingia kwa iPhone mpya sokoni na programu endeshaji mpya ya simu za iOs.

SOMA PIA  Facebook Messenger: Kuja na 'Option' ya kufanya mazungumzo baina ya mtu na mtu kuwa salama zaidi

Uwezo Wa Tachi Ya 3D

Hili sio la kushangaza sana kwani hata hapo awali wakati tunafanya tathimini ya simu za Apple zile za iPhone 6s na 6s Plus tulieleza kuhusu kipengele hiki

snapchat-press-and-hold

Kipengele Cha Tachi Ya 3D Kwa iOs Katika App Ya SnapChat

Katika simu hizo simu itachagua ifanye kitu gani kutokana na jinsi unavyobofya kioo cha simu yake ya iPhone. Jinsi ya kutumia kipengele hiki mtumiaji wa snapchat katika iOs itambidi abofye App hiyo kwa nguvu ili achague kama anataka kuongeza rafiki (Add a friend) au kama anataka kuchati na rafiki (Chat a friend).

SOMA PIA  WhatsApp kutuma data zako kwenda mtandao wa Facebook!

Mengi tumeona katika mtandao huu wa snapchat na hata hviyo inaonekana dhahiri kuwa App hii inapigana katika kuwa App namba moja na kuzipita zile nguli kama vile  WhatsApp na Instagram. Tuliona pia Snapchat ikiongeza kipengele kile cha kulipia ili kuangalia tena kama hukuona snap vizuri

Tuambie baada ya miaka mitano unaiona wapi hii App pia weka akilini muda ambao App hii umetumia kukuwa na kuwa katika ya App kumi bora za kijamii. Tuandikie sehemu ya Comment pia usisahau kutembele mtandao wako pendwa wa teknokona kila siku. TeknoKona Milele Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Comments

  1. […] post Tuangalie Maboresho Katika App Ya SnapChat! appeared first on […]

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania