Kama uko katika ulimwengu wa kibiashara kuna mambo mengi unayokutana nayo. Moja wapo ni kukutana na watu wapya karibia kila siku katika majukumu yako. Kwa wafanya biashara kitu cha kawaida kubalishana ni business card.
Business card ni njia nzuri ya kumkumbuka mtu na hata taarifa zake za mawasiliano — kama unakumbuka uliiweka wapi — Mara nyingie unaweza ukawe umeziweka katika waleti au hata mkoba wako mpaka zinajazana humu. La msingi ni kuziweka katika simu yako moja kwa moja
Kwa kupoteza muda unaweza ukaanza kuchukua kadi moja moja na kuanza kui save katika kitabu chako cha namba katika simu yako. Itakuchukua muda mpaka kumaliza kadi zote aua unaweza ukaiachia CamCard Free ikufanyie kazi zote hizo. Cha kufanya ni kupiga picha ya hiyo kadi tuu na App hii itahifanyi taarifa za mawasiliano za kadi hiyo katika simu yako au Tabiti.
Kwa mara ya kwanza App ya CamCard Free itakuruhusu ku save kadi 50 bure katika simu yako. Baada ya hapo itakubidi ulipie ili uendelee kutumia App hii. Baada ya kulipia unaweza chagua hadi ku save maelfu ya kadi katika simu yako.
Pia unaweza kutumia kadi (business card) ili kumtafuta mtu katika mitandao ya kijamiii kama vile LinkedIn, Facebook na Twitter. Kingine kikubwa ni kwamba, kama katika kadi hiyo kuna Anuani basi unaweza angalia muelekeo wa kufika katika eneo hilo ukiwa ndani ya App
SHUSHA APP HII
Kwa Android Hapa
Kwa iOs Hapa
One Comment