Skype imedumu kwenye ulingo wa biashara kwa miaka mingi na bado wanaendelea kuhudumia watu duniani kote hadi leo hii huku maboresho mbalmbali yakiendelea kutoka.
Skype imekuwa msaada mkubwa kwa miaka mingi kwa mashirika, makampuni na watu kwa ujumla wao duniani kote. Ushindani ni mkubwa na ingawa Zoom inaonekana kuwa maarufu zaidi lakini kuna watu/mashirika bado wanatumia Skype zaidi katika kufanya mawasiliano kwa njia ya mtandao.
WAtumiaji wa Skype nchini Marekani sasa wanaweza kupiga namba ya dharura (911) ya Polisi kupitia programu hiyo wezeshi na kuweza kupata msaada. Hii maana yake ni kwamba hata kama mtu amepoteza simu lakini anapata intaneti nyumbani kwake bado anaweza kupiga namba ya dharura na akapata msaada.
Kabla ya kuomba kumsambazia mtu sehemu uliopo Skype wameweka ujumbe wa tahadhari unasema kuwa shughuli haifanyi kazi sawa kama ambavyo mtu anatoa taarifa ya dharura kupitia simu ya kawaida.
Watu wote ambao watatumia Skype kupiga simu ya dharura wanashauriwa kuwepo maeneo ya nyumbani vinginevyo mtandao unaweza kudaka sehemu nyingine hivyo kumfanya asiweze kupata msaada aliohitaji.
Maboresho hayo ya kwenye Skype si kwa watumiaji wa nchini Marekani pekee bali hata Uingereza, Australia, Denmark na Finland. Teknolojia ndio hiyo inazidi kukua na makampuni wanatafuta ndio rahisi ya wateja wao kupata msaada wakati wa dharura.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
No Comment! Be the first one.